Bajaj zikiwa zimepakiwa na waendeshaji mjini Geita baada ya kuwa na madai ya kuonewa na askari. |
Bw. Joseph Dotto ambaye ni mwendesha bajaji
mjini Geita akilalamika juu ya kamata kamata ambayo inaendelea mjini humo.
|
Waendesha Bajaji Mjini
Geita Mkoani Humo wamelilalamikia jeshi la Polisi kuendelea kuwakamata
pasipokujua makosa yao ni nini na kujikuta wakishindwa kuendelea kufanya kazi
zao kwa amani hali ambayo imepelekea kutokuendelea na kazi zao za usafirishaji
wa abiria.
Wamesema hali hiyo
imeendelea kuwaathiri kutokana na wengi wao kukopa bajaji hizo na kutegemea
kufanya kazi hili waweze kurudisha madeni ambayo wanadaiwa na kampuni za
usafiri huo.
Bajaj
ndio usafiri maarufu mjini Geita kwa mizunguko ya hapa na
pale lakini Waendesha Bajaji wamejikuta wakisitisha kuendelea kufanya kazi zao
kutokana na kuwa na malalamiko ya kukamatwa na kutozwa faini kubwa
bila ya kujua makosa yao.
“Tumeendelea
kukamatwa na kupigwa faini pasipokujua makosa yetu ni nini hata tukiuliza
hatujibiwi tunakamatwa na kuambiwa twende kituoni tena na askari ambao wanakuwa
wamevaa nguo za kirahia je hiyo ni haki kweli sasa hivi ninasiku mbili sifanyi
kazi watoto wangu wamelala na njaa sijajua tatizo ni nini hadi kufikia hatua ya
kukamata bajaji zetu” Alisema Bw. Mussa Kisoke.
Hata
hivyo baadhi yao wameelezea kuwa pamoja na kukamilisha usajili wa bajaji zao na
kuwa na kila kitu bado wameendelea kukutana na dhoruba la kamata kamata
inayoendelea kwa sasa mjini humo.
“Sisi
hizi bajaji tumezikopa na tunarejesha marejesho kwa wiki na isitoshe zingine
zimekamilisha kila kitu kwa maana ya bima,Sumatra na leseni lakini tunakamatwa
na kupigwa faini kiuweli tunaumia sana” Alisema Joseph Dotto.
Kutokana
na malalamiko hayo kuliangukia Jeshi la Polisi kamanda wa Polisi
Mkoani Geita,Mponjoli Mwabulambo amesema msoko unaendelea kutokana na mambo ya
ukiukaji masuala ya usalama barabarani na kwamba wataendelea kuwakamata wale
wote ambao wameendelea kukiuka kanuni na taratibu za usalama Barabarani.
“Sababu
ni uwegeshaji hivyo barabarani kwa maana wanasimama sehemu ambazo sio sahihi
ninachotaka kusema kwamba hatuwaonei na tumeshakaa tukaongea nao maana
tumeshatoa elimu na utaki kutuelewa tutachukua hatua” Alisema Kamanda Mponjoli.
No comments:
Post a Comment