Mamlaka ya chakula na dawa nchini imewashauri
wananchi kuendelea kuepuka kubeba na kuhifadhi chakula cha moto kwenye mifuko
ya plastiki kwa madai kuwa mifuko hiyo ikipata joto hutoa kemikali ambayo
huingia kwenye chakula na kuleta madhara ya kiafya.
Rai hiyo imetolewa na mkurugenzi wa dawa na
vifaa nyongeza wa taasisi hiyo Bw.
Ansikari Fimbo katika kikao kazi cha wahariri na waandishi wa
habari wa mikoa ya Geita na Kagera kilicho fanyika kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa
wa kagera, kilicho lenga kuwataka wanahabari kuieleza jamii kuhusu
kazi zinazo fanywa na mamlaka hiyo.
Amewashauri baadhi ya wananchi kuacha mazoea
ya kubeba na kuhifadhi chakula chenye joto kwenye mifuko ya
plasitiki kwa kuwa mifuko hiyo ikichemka hutoa baadhi ya kemikali.
Aidha kwa upande wake meneja mawasiliano na
uhusiano wa umma wa mamlaka ya chakula na dawa nchini Bi Gaudencia Simwanza
ameiomba jamii kuendelea kushirikiana kwa kutoa taarifa pale wanapo baini uwepo
wa bidhaa feki za chakula dawa na vipodozi kwenye maeneo yao.
No comments:
Post a Comment