Halmashauri ya Wilaya
ya Geita imetoa kiasi cha Sh. Milioni 173.5 ikiwa ni mwendelezo wa halmashauri
kuhakikisha 10% ya makusanyo ya ndani inatolewa kwa vikundi vya wanawake,
vijana na walemavu ili kuweza kuvisaidia kujinyanyua kiuchumi kupitia shughuli
ambazo wamekuwa wakizifanya
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw. Ali Kidwaka ametaja changamoto ambazo wamekuwa wakikutana nazo katika zoezi hili ni pamoja na wakopaji kutokuwa na utayari wa kurejesha fedha hizo kwa wakati na wanakikundi kuhama kutoa eneo moja kwenda jingine bila ya kutoa taarifa
Aidha kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi amewasisitiza wajasiriamali hao kutokuwa na uwoga wa kukopa na pia kuzitumia fedha hizo kwa matumizi sahihi ya kujikwamua kimaisha
Mkuu wa Mkoa wa Geita Robert Gabriel ameziomba taasisi za kifedha kuendelea kutoa elimu ya utunzaji wa fedha ambapo
baadhi ya wanavikundi ambao wamepatiwa fedha hizo wameishukuru Serikali kwa namna ambavyo imeendelea kujitoa kuwasaidia Wananchi katika kujikwamua kimaisha.
No comments:
Post a Comment