Waziri wa Madini Mhe. Angellah
Kairuki akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya
Fedha ya Wizara hiyo kwa mwaka 2018/2019 leo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge
Uratibu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akitoa
maelezo Bungeni kuhusu hatua zitakazochukuliwa na Serikali katika
kuwalinda watoto wa kike ambapo ameahidi kuwa Serikali itatoa taarifa rasmi
kuhusu kuwepo kwa baadhi ya watu wanaowadhalilisha kijinsia watoto wa kike
na hatua zilizochukuliwa na Serikali.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza kuhusu mikakati ya Serikali kupambana na
Janga la Ukimwi hapa nchini ikiwemo kuhamasisha upimaji wa Virusi vya UKIMWI
hasa kwa wanaume kote nchini ili wajue hali zao na kuchukua hatua
stahiki.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali
Venance Mabeyo (wakwanza kushoto) akifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini Mhe
Angellah Kairuki Bungeni Jijini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idrissa Kikula
aliyesimama (kushoto) na Mmoja wa Makamishna wa Tume hiyo Prof. Abdulkarim
Mruma wakitambulishwa Bungeni leo mara baada ya kipindi cha maswali na majibu.
Sehemu ya Viongozi wa Tume ya Madini na wageni
mbalimbali wakiwemo wakuu wa Mikoa yenye madini wakifuatilia hotuba ya
Waziri wa Madini Bungeni Jijini Dodoma leo.
Sehemu
ya Wanafunzi waliofika Bungeni kwa ziara ya mafunzo wakiwa ndani ya ukumbi wa
Bunge wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
Serikali imesema kuwa pamoja na huduma za bidhaa ya fedha kuamuliwa na
nguvu ya soko kwa upande wake imekuwa ikichukua hatua za kisheria ili kuhakikisha
kuwa riba za mikopo zinapungua katika soko hapa nchini.
Hayo yameelezwa leo
Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Ashatu Kijaji
alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Konde, Mhe. Khatibu Haji juu ya Serikali
inachukua hatua gani ili benki ziweze kupunguza viwango hivyo vya riba
"Baadhi ya hatua
zilizochukuliwa na Serikali kupitia Benki Kuu ni pamoja na kuzitaka benki za
biashara kutumia mfumo wa kuhifadhi na kutoa taarifa za wakopaji (Credit
Reference Bureau System). Aidha, Benki hiyo imekuwa ikitoa mikopo ya muda mfupi
kwa benki za biashara kwa kiwango cha asilimia 6.89," amesema Dkt. Kijaji.
Dkt. Kijaji amezitaja
hatua nyingine zilizochukuliwa kuwa ni Benki Kuu kushusha riba (Discount Rate)
kutoka asilimia 16.0 hadi asilimia 9.0 pamoja na kupunguza kiwango cha chini
cha amana kinachotakiwa kuwekwa Benki Kuu na benki za biashara (Statutory
Minimum Reserve Requirememnt (SMR)) kutoka asilimia 10.0 hadi asilimia 8.0.
Vile vile Serikali
imeendelea kulipa malimbikizo ya madai yaliyohakikiwa kwa lengo la kupunguza
kiwango cha mikopo chechefu na kuchochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi.
Aidha, amesema baada
ya hatua hizo za kisera kuchukuliwa na Serikali, baadhi ya benki za biashara
hapa nchini zimeanza kupunguza riba za mikopo.
Ameongeza kuwa,
Serikali itaendelea kuchukua hatua za kisera ili kuhakikisha kuwa riba za
mikopo katika soko zinaendelea kupungua.
No comments:
Post a Comment