Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira kutoka Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS) Bibi Ruth Minja akiwasilisha mada wakati wa Warsha ya wadau
kuhusu hali ya upatikanaji wa Takwimu za viashairia vya mpango wa pili wa
maendeleo wa miaka mitano na malengo ya Kimataifa ya maendeleo endelevu usawa
wa kijinsia, utawala, amani na usalama Jijjini Dodoma.
Mtaalamu kutoka Taasisi
ya Africa Regional Manager, Global Partnership for Sustainable
Development Data Bw. Davis Adieno akiwasilisha mada katika Warsha
ya wadau kuhusu hali ya upatikanaji wa Takwimu za viashairia vya mpango wa pili
wa maendeleo wa miaka mitano na malengo ya Kimataifa ya maendeleo endelevu
usawa wa kijinsia, utawala, amani na usalama Jijjini Dodoma ikiratibiwa na
Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa Linaloshighulikia Usawa wa Kijinsia wa Wanawake (UN Women)
Bibi Usu Mallya akizungumzia maana ya takwimu za kijinsia
wakati wa Warsha ya wadau kuhusu hali ya upatikanaji wa Takwimu za viashiria
vya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano na malengo ya Kimataifa ya
maendeleo endelevu usawa wa kijinsia, utawala, amani na usalama Jijjini
Dodoma.
Meneja wa Takwimu za Bei
na Ajira kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bibi Ruth Minja
akiteta jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Ofisi hiyo Bw.
Said Ameir wakati wa wa Warsha ya wadau kuhusu hali ya upatikanaji
wa Takwimu za viashiria vya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano na
malengo ya Kimataifa ya maendeleo endelevu usawa wa kijinsia, utawala,
amani na usalama Jijjini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wa warsha ya wadau kuhusu
hali ya upatikanaji wa Takwimu za viashiria vya mpango wa pili wa maendeleo wa
miaka mitano na malengo ya Kimataifa ya maendeleo endelevu usawa wa kijinsia,
utawala, amani na usalama Jijjini Dodoma.
Mratibu wa Mpango Kabambe wa kuboresha na
kuimarisha Takwimu Nchini (Tanzania Statical Master Plan ) Bw.
Philemon Mahimbo akiwasilisha mada wakati wa wa Warsha ya
wadau kuhusu hali ya upatikanaji wa Takwimu za viashairia vya mpango wa pili wa
maendeleo wa miaka mitano na malengo ya Kimataifa ya Maendeleo
Endelevu, Usawa wa Kijinsia, Utawala, Amani na Usalama
Jijjini Dodoma.
Warsha ya Wadau
Kuhusu hali ya Upatikanaji wa takwimu za Viashiria vya Mpango wa Pili wa
Maendeleo wa Miaka Mitano na Malengo ya Kimataifa ya Maendeleo endelevu, usawa
wa Kijinsia, Utawala na Amani .
Akizungumza wakati wa
warsha ya siku mbili Mjini Dodoma Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira
Kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bibi Ruth Minja
amesema kuwa warsha hiyo ni muhimu na itasaidia katika
kubainisha maeneo yanayotakiwa kufanyiwa tafiti na kuzalisha takwimu
zitakazotumika katika kuchochea maendeleo mara baada ya kubaini maeneo ambayo
bado takwimu zake hazijakusanywa.
" Warsha
hii itatusaidia kuona ni wapi kuna takwimu ambazo hazijafikiwa kweye
maeneo mbalimbali ya kisekta ili ziweze kukusanywa na kusaidia katika kuleta
maendeleo" Alilisisitiza Bibi Ruth.
Akifafanua amesema
kuwa jukumu kubwa la Ofisi hiyo ni kukusanya na kuchambua na hatimaye kutoa
takwimu rasmi kwa ajili ya matumizi ya sekta mbalimbali ili kuchochea maendeleo
.
Kwa upande wake
mmoja wa wawezeshaji katika warsha hiyo Davis Adieno kutoka nchini Kenya
amesema kuwa wanapongeza hatua iliyochukuliwa ya kuwa na warsha hiyo ya wadau
kwa kuwa itasaidia takwimu zinazokusanywa zitasaidia wadau katika kupanga
mipango ya maendeleo.
Aliongeza kuwa wadau
wamekusanyika katika warsha hiyo ili kujifunza na wataweza kushiriki kikamilifu
katika kuondoa umasikini.
Naye Mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Usawa wa Kijinsia wa wanawake (
UN Women) Bibi Usu Mallya amesema kuwa uchambuzi wa Takwimu unasaidia kuonesha
upungufu wa takwimu zinazotakiwa kukusanywa katika sekta
mbalimbali.
Aliendelea kusema
kuwa Takwimu zilizopo zimenyumbulishwa kijinsia na kupitia warsha hiyo
washiriki wataweza kuendeleza takwimu za kijinsia.
Warsha ya ya Wadau
Kuhusu hali ya Upatikanaji wa takwimu za Viashiria vya Mpango wa Pili wa
Maendeleo wa Miaka Mitano na Malengo ya Kimataifa ya Maendeleo endelevu, usawa
wa Kijinsia, Utawala na Amani inafanyika mjini Dodoma kwa siku
mbili ikiwashirikisha wadau kutoka sekta ya umma , Binafsi na wadau mbalimbali
wa maendeleo.
(PICHA
NA FRANK MVUNGI- MAELEZO)
No comments:
Post a Comment