Waziri wa Nishati Dkt.
Medard Kalemani na Naibu Waziri Subira Mgalu wameongoza kikao kilichojadili
maendeleo ya Mradi wa Gesi ya Kusindikwa (LNG).
Kikao hicho kilifanyika
Aprili 30 mwaka huu Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma na kushirikisha
Mabalozi wa nchi za Norway, Uingereza na Uholanzi pamoja na Kampuni mbalimbali
za utafutaji wa mafuta kwa ajili ya Mradi wa LNG, Shirika la Maendeleo ya
Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati
(EWURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) na wataalamu
kutoka wizarani.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani na Naibu
Waziri Subira Mgalu (kushoto), wakiongoza kikao kujadili maendeleo ya Mradi wa
Gesi ya Kusindikwa (LNG), kilichofanyika Aprili 30 mwaka huu, Makao Makuu ya
Wizara Dodoma. Wengine pichani ni Mabalozi wa nchi za Norway, Uingereza na
Uholanzi, wawakilishi wa Kampuni mbalimbali za utafutaji wa mafuta kwa ajili ya
Mradi wa LNG, wajumbe kutoka TPD, EWURA na PURA.
Mabalozi wa nchi za
Norway, Uingereza na Uholanzi pamoja na wawakilishi wa Kampuni mbalimbali
za utafutaji wa mafuta kwa ajili ya Mradi wa LNG, wakiwa katika kikao hicho.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akisalimiana
na Mabalozi wa nchi za Norway, Uingereza na Uholanzi pamoja na
wawakilishi wa Kampuni mbalimbali za utafutaji wa mafuta kwa ajili ya Mradi wa
LNG, muda mfupi kabla ya kuanza kikao baina yao kujadili maendeleo ya Mradi
huo.
No comments:
Post a Comment