Mkurugenzi na Msajili wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali Bw. Marcel Katemba akizungumza na wadau Mashirika yasiyo ya
Kiserikali yanayotekeleza Sera zilizo chini ya Idara Kuu ya Maendeleo ya
Jamii Jijini Dodoma
Mkurugenzi
Msaidizi Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi Tausi Mwilima (kulia)
akieleza yatokanayo na kikao kilichopita kati ya Serikali na wadau wa NGOs
wanaotekeleza Sera mbalimbali zilizo chini ya Idara Kuu Maendeleo ya
Jamii Jijini Dodoma.
Mwakilishi kutoka Shirika la World Vision Tanzania
Bi Janeth Edson akitoa taarifa kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa hati ya
makubaliano ya utekelezaji wa Sera mbalimbali baina ya Serikali na NGOs kwa
upande wa NGOs katika kikao kati ya Serikali na wadau hao Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya
Maendeleo ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi akitoa mrejesho wa maendeleo ya
utekelezaji wa hati ya makubaliano na ushirikiano kati ya wadau wa NGOs baina
ya Serikali na NGOs kwa upande wa Serikali katika kikao kati ya Serikali na
wadau hao Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bw.
Patrick Golwike akitoa mrejesho kuhusu utekelezaji wa mpango wa kuamsha ari ya
wananchi kujitolea katika shughuli za maendeleo kwa wadau wa NGOs katika kikao
kati ya Serikali na wadau hao Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya
Mtoto Bi. Grace Mwangwa akitoa mrejesho kuhusu utekelezaji wa makubaliano na
wadau kuhusu utekelezaji wa Sera ya Mandeleo ya Mtoto kwa wadau wa NGOs katika
kikao kati ya Serikali na wadau hao Jijini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Idara Kuu
Maendeleo ya Jamii na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakifuatilia mada
mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika kikao kati ya Serikali na wadau wa NGOs
Jijini Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imeawataka wadau wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kuendelea kutekeleza Sera
mbalimbali zilizo chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii katika utekelezaji wa
majukumu yao.
Hayo yamesemwa
Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye pia ni Mkurugenzi na Msajili wa NGOs Bw.
Marcel Katemba Jijini Dodoma wakati wa Kikao kati ya Serikali na Wadau
hao kinachokaa kwa siku moja kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kazi zao na
kutekeleza Sera zilizo chini Idara kuu Maendeleo Jamii.
Ameongeza kuwa katika
kutekeleza Sera mbalimbali Serikali inashirikiana na Wadau mbalimbali wa
maendeleo nchini ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Amesema kuwa Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali yanafanya kazi kubwa nchini katika kuleta maendelo ya
jamii na Taifa katika sekta mbalimbali nchini.
“Wadau wa NGOs mnafanya
kazi nzuri na kubwa katika kuleta matokeo chanya kwa jamii na taifa letu”
alisisitiza Bw.Katemba.
Kwa upande wake
Mwakilishi Kutoka Shirika la World Vision Tanzania Bi. Janeth Edson akitoa
mrejesho wa makubaliano kati ya Serikali na NGOs kwa upande wa NGOs amesema
kuwa wao kama wadau wataendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza Sera
mbalimbali na kuwaasa wadau kuendelea kuunganisha nguvu na Serikali katika
kusogeza mbele gurudumu la maendeleo.
No comments:
Post a Comment