Kituo cha Sheria na
Haki za Binadamu (LHRC) imemtangaza Bi. Anna Henga kuwa Mkurugenzi mpya wa
kituo hicho ambapo atapokea mikoba ya Mkurugenzi wake wa muda mrefu, Dr. Helen
Kijo-Bisimba.
Uteuzi wa Bi. Henga ni
matokeo ya mchakato wa ndani wa muda mrefu uliotekelezwa na bodi ya Wakurugenzi
ya kituo hicho kutoka mwanzoni mwa mwaka 2017.
Katika taarifa
iliyotolewa leo na Kituo hicho imeeleaa kuwa uteuzi wa Bi. Henga unatarajiwa
kuanza Julai 1 mwaka huu..
Awali Bi. Henga
alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
No comments:
Post a Comment