Serikali imesema Juni
30, 2018 inatarajia kutoa ajira 10,140 za walimu wa shule za msingi nchini.
Hayo yamesemwa leo Mei
2, 2018 Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Tamisemi, Joseph Kakunda wakati
akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Ludewa (CCM), Deogratius Ngalawa.
Katika swali lake,
Ngalawa alitaka kupata majibu ya Serikali kuhusu upungufu wa walimu 500
wa shule za msingi na jinsi litavyoshughulikiwa.
Akijibu swali hilo,
Kakunda amesema; "Tunaendelea na mchakato kwa kushirikiana na Baraza la
Mitihani la Taifa kwa kupitia vyeti vya vya walimu na tunategemea ifikapo Juni
30 kuwaajiri."
No comments:
Post a Comment