Mgodi wa Dhahabu wa
Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS)
inatarajia kuzindua zoezi la upandaji wa mlima Kilimanjaro (Kilimanjaro
Challenge 2018), na kuendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa mwaka
2018 kwa ajili ya afua za UKIMWI nchini.
Shughuli hii
inatarajiwa kufanyika tarehe 4 Mei 2018 mwaka huu katika Hoteli ya Hyatt
Regency Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi katika
uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambapo atafanya zozezi la ugawaji wa fedha zilizokusanywa
mwaka jana 2017 zilizopatikana baada ya wadau mbalimbali kupanda na
kuendesha baiskeli kwa kuzunguzuka Mlima Kilimanjaro .
Kilimanjaro Challenge
against HIV & AIDS ni mfuko unaochangia juhudi za serikali katika
mapambano dhidi ya UKIMWI na kutoa elimu kwa jamii kuhusu maambukizi ya Virusi
Vya UKIMWI (VVU).
Kilimanjaro Challenge
ni mfuko muhimu unaoshirikiana na taasisi za nje na ndani ya nchi katika
kuendeleza mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI kwa jamii ya Kitanzania na Dunia kwa
ujumla ili kuwapa matumaini ya kuhakikisha jamii inabaki bila kuathiriwa na
VVU/UKIMWI katika miaka ijayo.
Mfuko huo pia unalenga
kuisaidia Serikali kukabiliana na VVU//UKIMWI sambamba na kutoa nafasi kwa
watalii wa ndani na nje kuupanda mlima Kilimanjaro.
Takwimu zilizotolewa
na Tume ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), zimeonesha kupungua kwa
maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka asilimia 5.1 % mwaka 2011/ 2012
hadi asilimia 4.7% mwaka 2016/17.
Kwa mujibu wa
Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt. Leonard Maboko anasema, “ Mwaka wa 2016,
inakadiriwa kuwa watu milioni 1.5 nchini wanaoishi na VVU na UKIMWI hadi
sasa watu 225
wanapata
maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa siku.
"Ugonjwa huu
umewaathiri zaidi vijana na watoto yatima zaidi. Tunahitaji kubadilisha hali
hii. Lengo la kukusanya fedha ni kuweza kusaidia serikali ya Tanzania katika
jitihada zake kufikia sifuri tatu.
"Sifuri katika
maambukizi mapya, sifuri ya unyanyapaa, sifuri katika vifo vitokanavyo na
UKIMWI. TACAIDS kwa kushirikiana na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) na wadau
wengine kwa kupitia mpango huu wa Kili Challenge tunapenda kutoa mchango na
ushirikiano wetu kwa Taifa ili kutunisha mfuko utakaowezesha kuendeleza
mapambano dhidi ya ugonjwa huu.
"Tuna matumaini
ya kujenga timu imara yenye hamasa ya kupambana na janga hili. Tunatoa wito kwa
makampuni na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi, wajitokeze ili
tusaidiaane kutunisha mfuko wa Kili Challenge na mwishowe kufikia malengo yetu
ya kuhakikisha tunakuwa na kizazi kisicho na maambukizi ya VVU/ UKIMWI,” Alisema Dkt. Leonard Maboko.
“Watoto watakaoshiriki
katika zoezi la Kilimanjaro Challenge mwaka huu ni wa kiume na wa kike wenye
umri kuanzia miaka 13. Watoto hao yatima kutokana na tatizo la VVU/ UKIMWI
wamesaidiwa na Kituo cha kulea watoto yatima cha Moyo wa Huruma Orphanage Center
kilichopo Geita.
"Changamoto kubwa
inayotokana na janga hili ni pamoja na maelfu ya watoto yatima wanaohitaji
misaada baada ya wazazi wao kufariki, wajane wasiokuwa na kipato, pamoja na
wazee wanaolazimika kuwalea wajukuu walioachwa na watoto wao ambao walifariki
kutokana kwa ugonjwa huo."
No comments:
Post a Comment