Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, akisoma hotuba ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha
2018/2019 bungeni jijini Dodoma.
Mapema leo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepisha kiasi cha
Shilingi Bilioni Mia Moja Sabini na Saba, Milioni Sita na Mia Mbili Thelathini
na Mbili Elfu.
Kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni Mia Moja Sitini na Sita, Milioni Mia
Sita na Sita, na Mia Mbili Thelathini na Mbili Elfu ni kwa ajili ya matumizi ya
kawaida, na Shilingi Bilioni Kumi na Milioni Mia Nne ni kwa ajili ya bajeti ya
maendeleo.
Prof. Adolf F. Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,(wa kwanza kushoto) akifuatilia
uwasilishwaji wa hotuba ya bajeti ya Wizara. Wa pili kutoka kushoto, ni Naibu
Katibu Mkuu Balozi Ramadhani Mwinyi akifuatilia hotuba.
Sehemu ya Watendaji wa Wizara wakifuatilia hotuba
ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019 iliyowasilishwa na kupishwa
bungeni jijini Dodoma
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akijibu maswali
bungeni mara baada ya kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha
2018/2019
Mhe. Dkt.
Susan Kolimba Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
(kushoto), akifuatilia hotuba ya bajeti bungeni jijini Dodoma.
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akifafanua
jambo mara baada ya kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara.
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisalimiana na Dkt. Stergomena Tax
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) walipokutana
katika viunga vya Bunge jijini Dodoma mara baada kuwasilisha hotuba ya bajeti
ya Wizara.
Mhe. Waziri Mahiga akijadili jambo na Mhe. Zitto
Kabwe Mbunge wa Kigoma Mjini katika viunga vya Bunge jijini Dodoma mara baada
ya kupitishwa kwa hotuba ya bajeti ya Wizara
Mhe. Waziri Mahiga na Mhe. Naibu Waziri Kolimba wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Waheshimiwa Mabalozi na Watendaji wa Wizara waliohudhuria tukio la uwasilishwaji wa bajeti ya Wizara bungeni jijini Dodoma
No comments:
Post a Comment