Watoto wakiwa kwenye shimo la kutupia uchafu
ndani ya mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM)wakiogota vyuma chakavu vinavyokuwa
vimetupwa na mgodi huo.
Afisa mahusiano wa mgodi wa GGM Mussa Shunashu akionesha maeneo ambayo ni hatarishi kwenye mgodi huo.
Eneo la kutupia taka kwenye mgodi wa dhahabu wa
Geita.
Bi. Sarah Kajoro akiwa kwenye masikitiko
kutokana na mtoto wake kushindikana na kujikuta akielekea maeneo ya mgodini.
Mzazi akijaribu kumwazibu mwanae kutokana na
kuwa na tabia ya kwenda kwenye maeneo ya mgodi wa GGM.
|
Mwenyekiti wa mtaa wa Kompaundi Edgha Onyango
akielezea hatua ambazo wameendelea kuzichukua dhidi ya wazazi ambao wamekuwa
wakiwaruhusu watoto wao kwenda maeneo ya mgodini.
Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl. Herman Kapufi
akikemea vikali tabia ya baadhi ya wazazi kuendelea kuwatumikisha watoto kuwa
watafutaji badala ya wao kutafuta.
|
Kumekuwepo na wimbi
kubwa la watoto kuingia kwenye maeneo ya mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM),kwa madai
baadhi yao wamekuwa wakitumwa na wazazi wao na walezi kwa ajili ya
kuokota vyuma chakavu na mawe ya dhahabu maarufu kwa jina la magwangala hali
ambayo inaweza kusababisha kutokea kwa hatari kwa watoto hao
kutokana na maeneo mengi kutokuwa salama.
Hali hiyo inatokana na
wazazi na walezi kushindwa kufuatilia kwa umakini muda wa wengi
kushindwa kujali masomo na kujikuta wakitumia njia za panya kuingia kwenye
mgodi huo uliopo wilaya ya geita kata ya mtakuja mjini humo.
Wakizungumza na
mtandao huu kwenye eneo la kutupia uchafu ndani ya mgodi huo baadhi ya
watoto hao wamesema kuwa wamekuwa wakiingia kwa ajili ya kuwinda wanyama pori
ambao wanapatikana kwenye maeneo ya mgodi huo.
“Sisi tunaingia humu
kwa nia tu ya kuwinda wanyama pori wala sio masuala ya kuogota vyuma na
mangwangala” Alisema mmoja wa watoto hao.
Afisa mahusiano wa
mgodi huo bw,Mussa Shunashu amewashauri watoto hao ambao wamekuwa wakiingia
kwenye maeneo hayo kuachana na tabia hiyo na badala yake watumie muda huo
kujisomea kwani kufanya hivyo wanaweza kujikuta wanaingia kwenye matatizo
kutokana na maeneo mengi ya mgodi kuwa hatari kwa maisha ya watoto hao.
Baadhi ya wazazi ambao
wamezungumza na mtandao huu umesikitishwa na kitendo cha watoto kwani wengi wao
wamekuwa wakitoroka nyumbani pasipo wazazi kujua wanakwenda wapi.
Mwenyekiti wa mtaa wa
kompaundi ambao unauzunguka mgodi huo,bw ediga Onyango,amewataka
walimu wakuu wa shule za msingi kutoa taarifa kwenye uongozi wa mtaa pamoja na
wazazi kuachana tabia ya kuwaagiza watoto kwenye maeneo ya mgodini.
Aidha mkuu wa
wilaya ya Geita Mwl,Herman Kapufi amewaonya wazazi wenye tabia hizo na kwamba
hatua kali zitachukuliwa kwa mzazi ambaye hatagundulika anamuagiza mtoto
wake kwenye maeneo ya mgodi wa GGM.
Takwimu za watoto
ambao wamekuwa wakiingia mgodini wa ggm zimeendelea kupanda ambapo kwa wastani
kila mwezi watoto sitini(60) wenye umri wa miaka sita na saba hadi
10 wameendelea kuingia kwenye maeneo hayo hatarishi.
No comments:
Post a Comment