Serikali imesema inapata tabu kukiri kuwa kuna hali ya njaa
nchini kwa kuwa mvua zimenyesha za kutosha mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa leo Mei 2, bungeni jijini Dodoma na Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji wakati akijibu swali la Mbunge wa
viti maalumu (CCM), Khadija Nasri Ally.
Mbunge huyo alitaka kujua kauli ya serikali kuhusu hali ya njaa
na umaskini nchini.
Alisema ripoti za Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Taasisi ya
utafiti (REPOA), zimebainisha kuwa hali ya njaa na umaskini imeongezeka mwaka
huu ikilinganishwa na miaka iliyopita.
Akijibu swali hilo Dk. Kijaji amesema hali ya njaa nchini haipo
kwani mvua za kutosha zimenyesha na wananchi wana amani kwani hakuna uhaba wa
chakula.
“Napata tabu kusema kusema hali ya njaa imeongezeka ndani ya
mwaka 2018 wakati mfumuko wa bei za bidhaa zinazochangia upatikanaji wa chakula
nchini kwa mwezi Machi mwaka huu ulikuwa asilimia 3.9 pekee.
“Hii ni dalili kuwa hali ya njaa nchini haipo labda mbunge
ametumia takwimu za miaka iliyopita mwaka 2016/17 ,” amesema.
No comments:
Post a Comment