Serikali imesema ipo
tayari kulipa deni la mikopo inayodaiwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii mara tu
baada ya Kanuni za kuunganisha mifuko ya Hifadhi za Jamii kupelekwa kwa wadau
ili kupata maoni yao na hatimaye zianze kutumika.
Akizungumza Bungeni Mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Fedha
na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji wakati akijibu swali la Mbunge wa Tumbe,Rashid
Ali Abdallah aliyetaka kujua ni lini Serikali itarejesha mikopo kwenye mifuko
ya hifadhi ya jamii.
“Mwaka 2016, Serikali ilifanya uhakiki wa deni
la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii linalotokana na mikopo ya uwekezaji kwenye miradi
mbalimbali ili kuandaa utaratibu wa malipo ambapo jumla ya deni
lililowasilishwa Serikalini kwa ajili ya uhakiki kwa mifuko yote ni shilingi
trilioni 2.1 na deni lililokubalika baada ya uhakiki ni shilingi trilioni 1.2”, Alisisitiza Dkt. Kijaji.
Akifafanua, Dkt. Kijaji alisema kuwa baada ya
uhakiki kukamilika, Serikali ilianza kuandaa utaratibu wa kulipa deni hilo kwa
kutumia hati fungani maalum zilizotarajiwa kuiva katika kipindi cha kati ya
miaka mitatu hadi 20.
No comments:
Post a Comment