Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya
Waandishi wakati akitoa tamko la ugonjwa wa Fistula katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Shirika
la AMREF Afrika Dkt. Floriance Temu akiongea
na waandishi wa habari wakati wa maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa fistula Duniani mbele ya mgeni rasmi Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto Dkt. Faustine
Ndugulile katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es salaam.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika
la kimataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA) Bi. Jacqueline Mahon
akiongea na waandishi wa habari mbele ya Waandishi wa habari na mgeni rasmi Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile.
Wanawake wajawazito wanatakiwa kuhudhuria
Kliniki mara kwa mara ili kuangalia maendeleo ya ujauzito wao na kupata vipimo na
matibabu kama itagundulika kuna uwezekano wa kupata ugonjwa wa Fistula.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
yaJamii, Jinsia,Wazee naWatoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa kutoa tamko la
ugonjwa wa Fistula katika kuadhimisha siku ya ugonjwa huo duniani.
“Asilimia 60 ya wanawake nchini ndiyo wanahudhuria
Kliniki mara kwa mara hii ni dalili mbaya kwani kama mwanamke mjamzito anaweza kuwa
na viashiria vya Fistula hatoweza kugundulika mapema na kupata matibabu na badala
yake asilimia 40 tu ndo wanaohudhuria Kliniki”
alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika
kutokomeza ugonjwa huo Serikali kupitia Wizara ya Afya imeandaa mkakati wa kupeleka
wataalam kwenye kila mkoa kujua idadi ya wagonjwa wa fistula ili kuweza kutokomeza
ugonjwa huo.
Vilevile Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali
imeimarisha na kukarabati vituo vya Afya vipatavyo 288 katika vitengo vya kuhudumia
wenye uzazi pingamizi kwani hiyo nayo ni sababu inayopelekea wanamke kupata
fistula.
Hata hivyo Dkt. Ndugulile amesema kuwa huduma
za Fistula zinapatikana Bure nchini hasa
kwenye hospitali za CCBRT, Bugando na Celian hivyo mwanamke akijiona ana dalili
za ugonjwa huo anatakiwa kuwahi katika kituo cha kutolea huduma za afya na kupata
Ushauri.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika lisilo
la Kiserikali linaloshughulikia mambo ya afya Dkt. Frolence Temu amesema kuwa katika
kupambana na ugonjwa wa Fistula nchini wanajenga uwezo kwa watumishi wa Hospitali
za Wilaya naMkoa.
Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Kimataifa linaloshughulikia idadi ya Watu UNFPA Bi. Jacqueline
Mahon amesema kuwa Shirika hilo limetoa mafunzo kwa watoa huduma za afya wapatao elfu nne ili kupambana na ugonjwa
huo.
“Mbali na kujengea uwezo watumishi hao pamoja
na ukarabati wa vituo vya afya ,watanzania wanatakiwa kuacha vitendo vya udhalilishaji
kwa wagonjwa wa fistula na wenye ugonjwa huu wajitokeze mara moja kwa ajili ya kupata
matibabu” Alisema Bi. Mahon.
Mbali na hayo Mkurugenzi Mkuu wa uendeshaji
hospitali ya CCBRT amesema inashirikiana na Serikali katika kupambana na ugonjwa
wa Fistula Hospitali yake inafanya matibabu kwa wagonjwa 1500 kila mwaka .
Ugonjwa wa Fistula huadhimishwa Mei 23
kila mwaka na maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kaulimbiu isemayo“BILA YA
KUMUACHA MWANAMKE YEYOTE MWENYE TATIZO LA FISTULA NYUMA SHARTI TUDHAMIRIE KUTOKOMEZA
FISTULA SASA”
No comments:
Post a Comment