Serikali mkoani Geita kupitia mradi wa
Tuimarishe Afya (HPSS) unaotekelezwa katika Mikoa mitatu hapa nchini kwa
kushirikiana na Serikali ya Uswis imekusudia kuendelea kupunguza
Changamoto za upatikanaji wa Dawa pamoja na Vifaa tiba kwenye Hospital,
Vituo vya Afya na Zahanati.
Aidha kwa upande wake Mshauri wa Menejimenti
ya dawa katika mradi huo Bi. Fiona Chilunda amesema mafunzo hayo yanajikita
katika malengo makuu matatu ambayo ni NHIF iliyo boreshwa , JAZIA pamoja na Matumizi
ya fedha kwenye Vituo vya Afya.
Kwa upande wa baadhi ya Washiriki wa Mafunzo
hayo akiwemo Mganga mkuu wa wilaya ya Chato Dkt. Athanas Ngambakubi na Kaimu Mganga mkuu wa wilaya ya
Bukombe Dkt. Irine Mkerebe wamesema kupitia
mafunzo hayo itasaidia kupunguza baadhi ya Changamoto katika Idara ya Afya
mkoani hapa.
No comments:
Post a Comment