Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Dkt. Akinwumi Adesina,
akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina
Khamis. Shaaban wakati wa Mkutano wa 6 wa jukwaa la ushirikiano kati ya Jamhuri
ya Korea Kusini na Magavana wa nchi za Afrika Jijini Busan-Korea
Kusini.
Makamu wa
Waziri Mkuu wa Korea ya Kusini Mhe. Kim Dog – Yeon (wa tatu kulia ) akiwa na
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Dkt. Akinwumi Adesina (kushoto)
wakati wa majadiliano ya fursa na changamato mbalimbali zilizopo nchi za
Afrika, Jijini Busan- Korea Kusini
Magavana wa nchi za
Afrika wametakiwa kuwa na utayari wa kuzisaidia nchi zao kutatua changamoto za
kiuchumi na kuhamasisha maendeleo endelevu ili kuendana na mapinduzi makubwa
yanayotokea kote Duniani kwa kuhamasisha ukuaji wa viwanda.
Rai hiyo imetolewa na
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika- AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina, wakati wa
Mkutano wa 6 wa jukwaa la ushirikiano kati ya Jamhuri ya Korea Kusini na Nchi
za Afrika uliolenga kujadili namna bora ya kuchochea ukuaji wa sekta ya viwanda
katika Nchi za Afrika.
Wadau wa Mkutano huo
uliofunguliwa na Makamu wa Waziri Mkuu wa Korea Kusini Bw. Kim Dog –
Yeon, wamezitaka nchi za Afrika kuhakikisha zinafanya mapinduzi ya
kiuchumi kwa kuwekeza kwenye viwanda na miundombinu kwa kuwa itasaidia
uchumi wa nchi kukua kwa kasi na kuleta maendeleo yenye tija.
Vilevile nchi za Afrika
zinahitaji kuwa na na ushirikiano wenye manufaa na wahisani ikiwemo nchi
ya Jamuhuri ya Korea Kusini ili kuharakisha maendeleo hayo ya
kiuchumi kwa kubadilishana uzoefu na kubaini fursa za ukuaji wa uchumi
utakaochochea ushirikiano huo.
Afrika inafursa nyingi
za kukuza uchumi kwa kuwa inarasilimali za kutosha kwa takribani sekta zote
muhimu za maendeleo ikiwemo ya madini, kilimo, mifugo na Uvuvi.
No comments:
Post a Comment