Nahodha wa zamani wa
Liverpool Steven Gerrard ametangazwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Rangers ya
Scotland kwa mkataba wa miaka minne.
Gerrard amechukua nafasi ya kocha Graeme Murty ambaye
amesitishiwa mkataba wake wa muda mfupi aliopewa wakati akichukua mikoba ya
Pedro Caixinha aliayefukuzwa kazi Oktoba mwaka jana.
Kiungo huyo mwenye heshima ya pekee kwenye
klabu ya Liverpool atakuwa na kibarua cha kurejesha ushindani dhidi ya
wapinzani wakuu wa Rangers nchini Scotland ambao ni Celtic.
Gerrard aliichezea Liverpool mechi 710 na
kushinda mataji 9 katika miaka 19 aliyoichezea timu hiyo. Pia nyota huyo mwenye
miaka 37 ameichezea timu ya taifa ya England mechi 114 na amewahi kuwa nahodha.
Mwenyekiti wa Rangers Dave King
ameeleza kuwa wao kama klabu wana imani kubwa na Gerrard, kwani tangu wameanza
maongezi naye amewaonesha ushirikiano mkubwa. Gerrard mwenyewe amesema
amefurahia uteuzi huo na atajitahidi kulinda heshima ya klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment