Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Andrew Chenge ameitaka Serikali kutekeleza agizo la Spika wa Bunge, Job Ndugai kuhusu kusuasua kwa miradi ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA).
Chenge ametoa kauli
hiyo leo Mei 2, bungeni jijini Dodoma baada ya kumalizika kwa kipindi cha
maswali na majibu ambapo wabunge wengi walisimama ili kuuliza maswali ya
nyongeza zaidi katika maswali yanayohusu Wizara ya Nishati.
Amesema serikali
inapaswa kufuatilia maelekezo ya Spika kwa kuwa lipo tatizo.
“Juzi Spika alielekeza
lakini angalieni wabunge waliosimama humu kuna tatizo! Nadhani serikali
ifuatilie maelekezo ya Spika, lipo tatizo haiwezekani.. angalieni, suala la
letter of credit (barua ya mikopo) ndiyo linasemwa na wakandarasi wote
hazijafunguliwa, letter of credit ni tatizo,” amesema.
Chenge alitoa
maelekezo hayo baada ya Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu kujibu swali la
Mbunge wa Morogoro Mashariki Kusini (CCM), Omar Mgumba aliyetaka kujua serikali
ina mkakati gani wa kuvipatia umeme vijiji vilivyorukwa na miradi wa REA III.
Naibu Waziri huyo
alisema mafaili yote ya wakandarasi yameshakusanywa na utaratibu wa kufungua
barua hizo za mikopo unaendelea sasa.
No comments:
Post a Comment