Mwenyekiti wa Chadema
Taifa, Freeman Mbowe ameeleza maneno ya mwisho aliyoambiwa na marehemu Kasuku
Bilago aliyekuwa Mbunge wa Buyungu mkoani Kigoma, ambapo alimwambia anahitaji
msaada wa haraka wa matibabu.
Akizungumza katika Ibada fupi ya kuuaga mwili wa marehemu Bilago, Mbowe amesema wakati alipokuwa nje ya nchi, nchini Afrika Kusini Bilago alimtumia ujumbe kwamba hali yake kiafya si nzuri hivyo anahitaji msaada.
“Nilipokuwa safarini
nchini Afrika Kusini, mwalimu Bilago aliniambia ninaumwa hivyo naomba ushauri,
nikawasiliana na bunge kuhusu taarifa yake ndipo walipomuamishia
muhimbilli.Mwalimu aliliona hilo kwamba alikuwa anahitaji msaada wa haraka wa
matibabu na kunitumia ujumbe nikiwa Afrika Kusini,” amesema Mbowe na kuongeza;
“Ndipo nilifunga
safari Ijumaa, Jumamosi nilienda Muhimbili, nilimkuta hali yake imebadilika
ghafla akakata kauli, nikaonana na madaktari ili wafanye juhudi za makusudi lakini
walijaribu kwa muda wa nusu saa lakini ilishindikana, mwenzetu alikuwa
ashatutoka na kutangulia mbele ya haki.”
No comments:
Post a Comment