Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akisisitiza kuhusu
umuhimu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa
Sheria, Kanuni na Taratibu na kuepuka vitendo vyote vya kuwabugudhi
wafanyabiashara wakati wa kutekleza jukumu la kukusanya kodi katika maeneo yote
nchini wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu leo
Bungeni Jijijni Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job
Ndugai akisisitiza jambo wakati akijibu miongozo ya wabunge leo
Bungeni Jijini Dodoma mara baada ya kipindi cha maswali na majibu.
Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akiwasilisha hotuba ya
makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019 leo
Bungeni Jijini Dodoma.
Sehemu ya wageni waliofika bungeni wakifuatilia kipindi cha
maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akitoa maelezo kuhusu
hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kufikisha huduma za maji kwa wananchi
kote nchini.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza kuhusu taratibu za matibabu hasa kuhusu
kitendo cha baadhi ya viongozi kuonyesha mfano katika kutoa chanjo cha
wasichana wenye umri wa miaka kuanzia 14 ili kuzuia saratani ya mlango wa
kizazi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.
Mbunge wa viti maalum
(CCM) Mhe. Amina Mollel akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali
katika kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanajengewa mazingira rafiki
yatakayowawezesha kushiriki katika ujenzi wa uchumi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi kukaa pamoja na chama cha wapangaji wa nyumba za
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ili kusikiliza changamoto zao pamoja na kutoa
fursa kwa wapangaji wa muda mrefu kununua nyumba hizo.
Mhe. Majaliwa ametoa
tamko hilo leo Bungeni, Jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa
Ilala Mhe. Azzan Mussa Zungu juu ya lini Serikali itakutana na wanachama na
wamiliki wa nyumba za NHC ili kutoa fursa kwa wapangaji wa muda mrefu kuzinunua
nyumba hizo badala ya kuwaondoa.
"Shirika la nyumba
inayo sera inayotoa muongozo namna nyumba hizo zinavyotakiwa kutumika ikiwemo
na maamuzi kwa wale wanaokaa kwa muda mrefu kwenye nyumba hizo inapofikia thamani
ya nyumba kushuka iweze kurasimishwa rasmi ili kutoa fursa kwa wapangaji hao
kuweza kuzinunua kwa kulipa kiwango kidogo kidogo," alisema Waziri Mkuu.
Aliendele kusema,
asilimia kubwa ya wapangaji wa muda mrefu wa nyumba hizo ni wastaafu ambao
hawana nyumba. Hivyo ameitaka NHC kuangalia jambo hilo na kuwapa fursa
wapangaji hao kulipa kidogo kidogo kadiri ya uwezo wao.
Wakati huo huo Waziri
Mkuu ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutotumia lugha ya kuudhi au
kutumia nguvu pindi wanapokusanya kodi kwa wafanyabiashara. Badala yake
wawaelimisha wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kulipa kodi na kuwaeleza ni kwa
kiasi gani kodi hiyo imefikia.
Amesema hayo, alipokuwa
akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Tunduma Mhe. Frank Mwakajoka kuhusu kauli
ya Serikali juu ya usumbufu unaoletwa na TRA kwa wafanyabiashara wakati wa
kukusanya kodi.
"Serikali imeunda
chombo cha kusikiliza kero za wananchi ndani ya TRA lakini kama hawatasikilizwa
wanauwezo wa kupeleka kero zao Wizara ya Fedha au kwa kiongozi yoyote mkubwa katika
eneo lake kama vile Mkuu wa Mkoa au Wilaya," alisema Waziri Mkuu.
Aidha ameitaka Mamlaka
hiyo kufanya kazi kwa weledi na kuwa na mazungumzo na wafanyabiara. Pia
tathmini ya kodi isiwe kiwango kikubwa kuliko mtaji wa mfanyabiashara.
Hata hivyo amesema hatua
zitachukuliwa kwa yeyote ambaye hatatumia utaratibu mzuri wa kukusanya
kodi na amewataka wafanyabiashara kufanya biashara kwa amani.
No comments:
Post a Comment