Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, amewajia juu baadhi ya watumishi wa serikali ambao wanatabia ya kuwafukuza kazi walimu wakuu wa shule ambao hutoa matokeo mabaya katika mitihani ya Taifa.
Na kuongeza watumishi hao hasa maofisa elimu,
wanajukumu la kusimamia elimu katika eneo husika na sio kuwatupia lawama walimu
pindi matokeo yanapokua mabaya.
“Hiyo sio sawa ni uonevu kwa wakuu
wa shule kwa sababu na wenyewe wana viongozi juu yao, kwa nini wao ambao
wanatakiwa kuwasimamia wasiwajibishwe, ninaagiza maofisa elimu wafanye kazi yao
vizuri, utakuta mtu ana shule tano unashindwaje kuzisimamia, kwa hiyo katika
hili serikali itahakiksha tunaimarisha usimamizi ikiwa ni pamoja na kuondoa
viongozi ambao ni mizigo” amesema
Ndalichako
Ndalichako ameongeza kwamba kama serikali
inachukua hatua kubwa ili kuimarisha ubora wa elimu lakini baadhi ya watendaji
hao wamekua wakirudisha nyuma jitihada hizo na serikali haitasita kuchukua
hatua kwa watendaji hao.
Kwa upande mwingine Waziri Ndalichako ameitaka
Tume ya Elimu ya Vyuo Vikuu (TCU) pamoja na Baraza la Taifa la Mafunzo ya
Ufundi (NACTE) kuhakikisha wanafuatilia ubora elimu ya juu ili kutoa wahitimu
wenye sifa zinazostahili na kiwango cha elimu husika.
No comments:
Post a Comment