Wavuvi wa
mwalo wa Makatani kata ya Nkome wilayani Geita wakiendelea na maandalizi
kwaajili ya kwenda kwenye shughuli ya uvuaji wa dagaa.
Zana za uvuvi ambazo wamelalamikiwa kuwa
zinakamatwa na maafisa uvuvi kwa madai kuwa zinashiriki kwenye suala la uvuvi
haramu.
|
Mzee Yohana Kulwa akielezea masikitiko yake
kutokana na suala kuendelea kukamatwa na kupigwa faini na watu wa idara ya
uvuvi bila ya kuwa na makosa yoyote.
|
Wavuvi wa Mwalo wa
makatani Kata ya nkome Wilaya na Mkoa wa Geita,wamelalamikia kuonewa na watu
kutoka idara ya uvuvi kutokana na kuendelea kuwakamata na kuwapiga faini
pasipokuwa na makosa yoyote hali ambayo imeendelea kuwatia hofu pindi
wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao.
Hatua hiyo imekuja ni
kutokana na msako ambao unaendelea ziwa Viktoria wa kuwakamata watu ambao
wameendelea kujihusisha na shughuli za uvuvi haramu.
Wakizungumza na Mwaandishi wetu baadhi ya wavuvi hao wamesema kuwa pamoja na kuendelea kutii
sheria kwa kutumia zana za uvuvi ambazo zinakubalika kwa mujibu wa sheria bado
wameendelea kukamatwa na kupigwa faini na watu wa idara ya uvuvi.
Mwenyekiti wa
kitongoji hicho Bi. Anna Peter na Mwenyekiti wa BMU Bw,Peter John wamedai
kutokushirikishwa kwenye shughuli hiyo ya kukamata watu hao na kwamba
elimu bado ni tatizo kwa wavuvi wengi kutokujua ni zana zipi ambazo
zinatumika kwenye shughuli zao kutokana na kutokupewa elimu.
Hata hivyo kwa upande
wake diwani wa kata hiyo,Masumbuko Nsembe amesema malalamiko ya wavuvi hao
amekwisha kuyapeleka halmashauri na kwamba hadi sasa yanafanyiwa kazi.
Mtandao huu
umemtafuta Mkuu wa oparesheni hiyo,Bw Roman Mkenda kwa njia ya simu ambapo
amesema kuwa baadhi ya wavuvi wamekuwa wakikimbia pindi wanapowaona
hali ambayo inasababisha wao kujua kuwa ni mvuvi haramu na kwamba
suala la elimu wamekuwa wakilitoa pindi mtu anapoomba kibali cha kutaka kuwa
mvuvi.
No comments:
Post a Comment