Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Augustine Mahiga amesema Watanzania waishio
nje ya nchi wanatuma zaidi ya Sh trilioni moja nchini kwa mwaka.
Waziri Mahiga ametoa
taarifa hiyo bungeni jijini Dodoma leo Mei 23, wakati akiwasilisha bajeti ya
wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/19.
“Watanzania hao
wamekuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa taifa kwa kuwa baadhi yao wamenunua
nyumba zenye thamani ya Sh bilioni 29.7 kutoka Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC).
“Aidha, katika sekta
ya afya, timu ya madaktari wa Kitanzania waishio Marekani kupitia taasisi ya
afya, elimu na maendeleo ilitoa huduma ya afya bila malipo na vifaa tiba,”
amesema.
Pamoja na mambo
mengine, Waziri Mahiga amesema Tanzania kama nchi huru haiwezi kuchaguliwa
maadui na marafiki duniani na kwamba itaendelea kushirikiana na mataifa
mbalimbali duniani kulingana na jinsi itakavyoona inafaa.
No comments:
Post a Comment