Friday 26 February 2016

WATU WANNE WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA BASI LA MASHIMBA EXPRESS.


          Baadhi ya watu waliojitokeza katika eneo la tukio pamoja na abiria walionusurika.
 
                    Basi la mashimba express baada ya kugongana na gari dogo.
                          Gari dogo lililogongana na basi la mashimba express.

Watu wanne wafariki dunia katika ajali baada ya basi la Mashimba Express lililokuwa linasafiri kutoka Kahama kuelekea  jijini Mwanza kugongana na gari dogo katika eneo la njia panda kuelekea wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga.


Ajali hiyo imetokea jana jioni ambapo mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa ilisababishwa na gari ndogo iliyokuwa katika mwendo kasi ambayo ilipoteza uelekeo na kisha kuligonga basi hilo.Watu wawili waliokuwa katika gari hilo akiwemo dereva walifariki dunia papo hapo

Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt Albert George Masigati amesema kati ya saa 12 na saa moja usiku wa kuamkia leo walipokea miili ya marehemu wanne katika hospitali hiyo ,wote wakiwa ni wanaume na majeruhi wanane,kati yao wanawake wanne na wanaume wanne.

Hata hivyo Dkt Masigati amesema huenda idadi ya majeruhi ikaongezeka kutokana na taarifa kuwa baada ya ajali hiyo kutokea baadhi ya majeruhi walikimbizwa katika hospitali ya Kolandoto na Kishapu.

Dkt Masigati amesema hakuna majeruhi aliye katika hali mbaya na kwamba bado wanaendelea kuwafanyia uchunguzi 

No comments:

Post a Comment