Sunday 28 February 2016

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA, KUTUA JIJINI MWANZA KESHO KUTWA.

         Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Kassim Majaliwa.
                   Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  Baraka Konisaga.

Wakazi  wa Jiji la Mwanza na vitongoji vyake wametakiwa kujitokeza kwa wingi keshokutwa ili kumpokea Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye anatarajiwa kuwasili jijini hapa akitokea jijini Dar es Salaam akielekea mkoani Simiyu.

Hayo yameelezwa jana jijini hapa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Baraka Konisaga ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, wakati alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara wa Kamanga Feri wakati alipowaongoza kwenye shughuli ya kufanya usafi.


“Niwataarifu kuwa Waziri Mkuu atawasili jijini Mwanza kwa mara ya kwanza siku ya Jumanne majira ya saa 7:00 mchana akitokea jijini Dar es Salaam… akishawasili hapa ataelekea mkoani Simiyu kikazi, nawaomba muiweke moyoni siku hiyo ya Jumanne na mjitokeze kwa wingi kumlaki kiongozi wetu mpendwa, ” alisema.

No comments:

Post a Comment