Kutokana na baadhi ya magari ya kusafirisha
abiria kuwaka moto na kusababisha ajali jeshi la zima moto mkoani
Geita limeendelea kutoa elimu kuhusiana na matumizi ya kifaa cha kuzimia
moto (fire extinguisher) katika magari ili
kuzuia ajali za moto katika magari yao.
Storm habari
imezungumza na mkufunzi wa mafunzo hayo wa jeshi la zima moto Ibrahimu Kamonja
ambapo amesema kuwa lengo la kutoa
mafunzo hayo ni kuwasaidia madereva wote wasiojua matumizi ya kifaa hicho ili
kuwasaidia wapatapo tatizo hilo.
Kwa upande mwananchi aliyeshuhudia mafunzo hayo musa kitinde
amesema utoaji huo wa mafunzo ni mzuri na utawasaidia madereva hao kujua jinsi
ya kutumia kifaa hicho pindi wapatapo
ajali zitokanazo na moto katika magari yao.
Hata hivyo mmoja wa madereva hao Musa James
amesema kuwa ameipokea vizuri elimu hiyo na kwamba ataifanyia kazi baada ya
kuipata.
Mwenyekiti wa chama hicho cha madereva mkoani
faustine john amelishukuru jeshi la zimamoto mkoani hapa kwa kuendelea kutoa mafunzo kabla ya kutoa
adhabu.
No comments:
Post a Comment