Thursday 25 February 2016

WAFANYABIASHARA WA MAZAO MKOANI GEITA KUTUMIA MIZANI KUNUNULIA BIDHAA NA SIYO MADUMU.

    Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mh.Doto Biteko na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa            Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.

Kilio na Masikitiko kilimfikia Mbunge wa Jimbo la Bukombe  Mh Doto Biteko
kutoka kwa wakulima wilayani Bukombe Mkoani Geita kwamba

wafanyabiashara wa mazao wanatumia madumu makubwa maarufu kama

mozambiki kuwaibia mazao yao na kumtaka awasaidie ili kunusuru mazao

yao.

Baada ya kupokea kilio hicho cha wakulima  Biteko aliwakilisha
hoja hiyo kwenye baraza la madiwani ambapo madiwani nao walimuunga
mkono na kuungana naye kuwa hata wao wamepelekewa malalamiko hayo na
wananchi kuwa wizi uliokithiri dhidi ya mazao yao kutokana na
umaskini walionao na kupelekea hali ya kunyonywa..


Katika hatua nyingine Biteko alisema kwa hali hiyo wafanyabiashara hao
wanaotaka utajiri mkubwa kwa njia zisizo sahihi  kamwe hawezi

kuvumilia hivyo amewataka wafanye biashara iliyo halali na wapate

utajiri ulio halali na si vinginevyo.

Aliongeza pia eneo ambalo wananchi wananyanyasika sana 

ni kata ya Bulega na vijiji vyake ambao ndiyo walikuwa
wakwanza kumpelekea malalamiko .


Diwani kata ya Lyambamgongo Bw. Boniphace  Shitobelo alisema tatizo la

Madumu ni la wilaya nzima hivyo wameitaka halmashauri ichukue hatua

kwa wafanyabiashara hao wezi na suluhu la  tatizo hilo ni
kuhakikisha mazao yote yananunuliwa kwa mizani na si kutumia
Madumu.


Akihitimisha mjadala huo mwenyekiti wa halmashauri Bw.Safari  Mayala kwa
niaba ya Baraza limemuagiza Mkurugenzi ahakikishe analifanyia kazi

suala hilo kupitia kwa Afisa Biashara na Afisa kilimo wamuandikie

barua mkuu wa Polisi wilaya (OCD) ili washirikiane kuwakamata
wafanyabiashara hao.


Safari aliongeza kuwa  Baraza hilo limeazimia kuwa ni marufuku katika Wilaya

ya Bukombe kwa mfanyabiashara yeyote wa mazao kununua mazao kwa mkulima

kwa kutumia madumu ya aina yeyote, na badala yake  watumie

mizani.

 Pia Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo James Ihunyo aliwaeleza

madiwani kuwa atatekeleza agizo hilo la kumuandikia barua OCD na

atahakikisha Afisa biashara akishirikiana na watendaji wa kata na
vijiji  wanalisimamia zoezi hilo.

No comments:

Post a Comment