Tuesday 23 February 2016

WAKAZI WA MKOA WA GEITA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA.


Naibu waziri wa ardhi ,nyumba na manendeleo ya makazi,Mh,Angelina Mabula.

Wananchi mkoani Geita wametakiwa kuchangamkia fursa katika maeneo ambayo  yameshatengwa na serikali ikiwa ni pamoja na kupanga au kununua nyumba za shirika la nyumba la taifa zilizopo  katika kata ya bomba mbili Mkoani hapa.

Rai hiyo imetolewa na Naibu waziri wa ardhi ,nyumba na manendeleo ya makazi,Mh,Angelina Mabula katika ziara yake ya siku moja Geita, ambapo amesema kuwa kutokana na mji wa Geita  kukua  kwa kasi kubwa ni vyema wananchi  kutumia fursa zilizopo  ikiwa ni pamoja na kuchukua maeneo yaliyowazi kwa ajili ya makazi.

Aidha kwa upande wake  meneja wa kanda mwandisi,Benedict Kilimba,amesema kuwa mradi na ujenzi wa nyumba za gharama nafuu unaendeshwa kutoka mkoa wa Mwanza kwa wilaya ya Geita na  wilaya ya chato unaendeshwa kwa kutumia mkoa wa kagera.


 Msimamizi wa mradi huo Julius Ntoga,ameelezea namna na jinsi mradi huo ulivyotekelezwa kwa  kushirikiana na Halmashauri ya mkoa wa Geita.

No comments:

Post a Comment