Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt.
Medard Kalemani, (wa kwanza kushoto), akiongozwa na Meneja Mwandamizi Miradi ya
Umeme wa TANESCO pamoja na wafuasi wengine.
Mbunge wa geita mjini Mh Costantine Kanyasu
Wananchi wa kata ya
mtakuja mtaa wa Nyamalembo, Katoma na
Kompaund, wamefikisha malalamiko yao kwa
Naibu Waziri wa nishati na madini,mh Dr.Medadi Kalemani juu ya nyumba zao kuendelea kubomoka kutokana na upasuaji wa miamba unaofanywa
na kampuni ya uchimbaji wa madini ggm mkoani Geita.
Wakizungumza
katika ofisi za serikali ya mtaa
wamesema kuwa ni vyema kwa naibu waziri kuangalia uwezekano wa kuhakikisha kuwa
wanadhibiti swala la milipuko ambayo imekuwa ikitokea mara kwa mara na
kusababisha athari zikiwemo za kiafya na kuharibika kwa majengo.
Aidha Dr,Medadi Kalemani amewaomba wananchi kuwa wavumilivu
na kwamba swala hilo kuaniza jumatatu ya wiki ijayo litafanyiwa kazi na wizara hiyo kwa kupitia mtafiti wa
serikali.
Katika hatua
nyingine mbunge wa geita mjini Mh
Costantine Kanyasu amemshukuru naibu
waziri kwa kufika na kujionea namna na jinsi ambavyo wananchi wamekuwa
wakiathirika kutokana na milipuko hiyo.
No comments:
Post a Comment