Saturday 27 February 2016

BARAZA LA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA LIMEPITISHA SH.BILIONI 69.6 KWA MWAKA WA FEDHA 2016 NA 2017.


Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Geita.

Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani hapa limepitisha sh.bilioni 69.6 katika mapendekezo na mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2016 na 2017.

Akiwakilisha bajeti hiyo ya mwaka 2016/ 2017,Afisa mipango wa wilaya Mh.Duncan Thebas amesema kuwa bajeti hiyo imezingatia mambo ya msingi ikiwa pamoja na mwongozo wa serikali wa namna ya kuandaa bajeti  ikiwa ni pamoja na mpango wa kukuza uchumi na kuondoa umasikini.

Wakizungumzia  swala la ukusanyaji wa mapato ndani ya wilaya kwa upande wa madiwani  wameendelea kulalamikia juu ya makapuni yaliyo ndani ya mgodi wa dhahabu (GGM),kutokuwa na tabia ya kuchangia ushuru na wale ambao wamekuwa wakifanya shughuli  za uchanjuaji.

Afisa mipango Thebas amejibu juu ya swala la baadhi ya makampuni kutokulipa kodi ni kutokana na wengi kutokuwa na mikataba ya muda mrefu wa kufanya kazi katika mgodi huo.

Mwenyekiti wa halmashauri ya mji Elisha Lupuga,ameweza kuipitisha bajeti hiyo ambayo asilimia kubwa ya madiwani wameweza kuiunga mkono.

No comments:

Post a Comment