Raisi mstaafu wa awamu ya nne(kushoto)Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Raisi wa awamu ya tano(kulia)Dkt.John Pombe Magufuli.
Moja kati ya hoja zinazogonga vichwa vya baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni
mabadiliko ya Uenyekiti wa Chama hicho ambayo yatamuwezesha mzee wa Kutumbua Majipu, Rais John Magufuli kuanzisha operesheni hiyo ndani ya chama hicho.
Mwenyekiti wa CCM,
Jakaya Kikwete amesema kuwa ataachia nafasi hiyo hivi karibuni na kumkabidhi
Rais Magufuli, lakini alitoa angalizo kuhusu uhusika wake kwenye chama hicho
baada ya kujivua kofia hiyo nzito.
Ingawa Katiba ya Chama
hicho inaeleza kuwa mwenyekiti mpya atapatikana mwaka 2017, Mwenyekiti wa Chamo
hicho, Dk. Jakaya Kikwete amepanga kuachia nafasi hiyo mapema (mwaka huu) kama
ilivyokuwa kwa watangulizi wake.
Akiongea jana kwenye
uzinduzi wa Kitabu cha maisha ya kada maarufu wa chama hicho, Marehemu Captain
John Komba, Dk. Kikwete alieleza kuwa ataachia nafasi hiyo lakini hataacha
kushiriki vikao vya ndani na mambo ya maamuzi ya chama hicho.
“Uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
nitaachia, lakini mambo ya ndani yanayohusu chama hiki sitaacha kushiriki,”
alisema.
No comments:
Post a Comment