Mgodi wa Geita Gold Mine(GGM)
Wakazi wa mitaa ya Nyamalembo ,Compound na Katoma mkoani
Geita wameulalamikia mgodi wa Geita gold mine (GGM) kutokana na kuweka bikoni
katika maeneo ya makazi yao zikionyesha kuwa eneo hilo ni mali ya mgodi huo hali
ambayo imesababisha wananchi hao kushindwa kuendelea na shughuli zao za maendeleo.
Hayo yamebainishwa leo na wakazi wa maeneo hayo katika
ziara ya naibu waziri wa nishati na madini alipotembelea maeneo hayo ili kujionea
adha hiyo huku wakimuomba kulichukulia hatua za haraka jambo hilo.
Kwa upande wake kaimu Afisa mahusiano wa mgodi huo Bw.Simon
Shayo amesema kuwa kampuni hiyo haitambui madai hayo jambo ambalo limewashangaza
wanachi wa maeneo hayo kutokana na kuzuiwa kufanya shughuli zao kwa muda mrefu.
Hata hivyo baada ya afisa huyo kukana kuwa kampuni haitambui
zuio hilo naibu waziri wa nishati na madini Mh.Medadi Kalemani amewaagiza wananchi
wamaeneo hayo kuendelea na shughuli zao huku akidai kuwalipa
fidia wale waliokuwa wakidai kuzuiwa kufanya shughuli zao pindi mgodi utakapohitaji
maeneo hayo.
Aidha ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kushirikiana
na viongozi kushughulikia suala la maendeleo kwani kufanya hivyo itasaidia kuongeza
chachu ya maendeleo mkoani hapa na taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment