Thursday 25 February 2016

GARI LAPINDUKA MKOANI GEITA NA KUPELEKEA KIFO CHA MTU MMOJA NA MAJERUHI WAWILI.



Kamanda wa polisi mkoani Geita,Mponjoli Lotson

Mtu  mmoja  ambaye hajafahamika  jina lake  amefariki  dunia  baada ya gari alilokuwa amepanda kuacha  barabara na kupinduka hadi   kupelekea  kifo chake .

Aidha ajali hiyo imetokea  jana tarehe 24/02/2016 majira saa tatu na dakika 5 usiku eneo la kijiji cha Chibingo barabara ya Geita katoro kata ya mtakuja wilayani na mkoani hapa, gari  hilo lina  usajili  no t566cvv Toyota Noah mali ya Rhoda Mussa  mkazi wa Sengerema.

Gari hilo lilikuwa likitokea Geita kuelekea Chato na  lilikuwa likiendeshwa na Boniphace Alex  mwenye umri wa miaka 21 mkaazi wa muungano Chato.

Gari liliacha barabara kisha  kupinduka  na kusababisha kifo cha mtu huyo ambaye hajafahamika jina  lake na anasadikika kuwa na umri kati ya miaka 22-25  pia ilipelekea   majeruhi kwa abiria wawili  ambao walikuwa ndani ya gari hilo waliofahamika kwa majina  Mathias Pius mwenye umri wa miaka 27 ambaye ni  mkulima wa katoro  na Leornad Beatus mwenye umri wa miaka  40 ambaye ni  mkaazi wa chato.

Majeruhi wote wana majeraha sehemu mbalimbali ya miili yao  na wamelazwa hospitali ya rufaa  Geita  lakini mwili wa marehemu ambaye  hajafahamika jina una jeraha kichwani  na umehifadhiwa  chumba cha kuhifadhia maiti hosptalini hapo.
 
Aidha chanzo cha ajali hiyo ni  mwendo kasi,  mtuhumiwa Boniphace amekamatwa.

Kamanda wa polisi mkoani Geita,Mponjoli Lotson amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo,  hivyo jeshi la polisi linatoa onyo  kwa madereva wote kuwa makini na kufuata  taratibu na kanuni  za usalama barabarani.

No comments:

Post a Comment