Friday 19 February 2016

WATOTO WANNE WA FAMILIA MOJA WENYE ULEMAVU WA VIUNGO MKOANI GEITA WANAHITAJI MSAADA.

                   
                      Watoto wa mzee Shikome Saliboko wenye ulemavu.

            Mtangazaji wa Stormfm(kati) Joel Maduka akiwa pamoja na watoto wenye ulemavu.

                      
                        Watoto wa mzee Shikome Saliboko wenye ulemavu.

Famila ya Shikome Saliboko yenye watoto wanne ambao wote ni walemavu wa viungo wanaomba msaada kwa wasamalia wema ambao wataguswa  kuwasaidia misaada mbali mbali ikiwa ni pamoja na kupatiwa elimu na mahitaji mengine.


Storm habari ilifika kijijini hapo na kuzungumza na kaka wa watoto hao Costantine Kizalia amesema kuwa tangu kufariki kwa baba yao mzazi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto za kimaisha moja wapo ni kukoswa mahitaji ya kila siku ikiwemo  mavazi,chakula na masomo.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake Saimon Shikome ambae ni mlemavu amewaomba wananchi wenye mapenzi mema pamoja  na serikali kuwapatia msaada wa kielimu kwani wanaamini elimu ndio msingi pekee ambao utawawezesha kupiga hatua za kimaisha.


Kwa upande wake mtendaji wa kijiji hicho Ugugwe Isalika,amesema kuwa mpaka sasa bado wanaendelea na jitihada  za kuhakikisha kuwa watoto hao wanapatiwa misaada lakini pia amewaomba wananchi kujitoa kwa hali na mali kuwasaidia.

No comments:

Post a Comment