Taasisi ya kuzuia na kupamba na rushwa(Takukuru)
imewafikisha mahakamani mhandisi wa halamshauri ya wilaya ya Geita na
mkandarasi kwa makosa ya rushwa.
Akisoma makosa hayo mbele ya hakimu
mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ,Mh.Ushindi Swalo mwendesha mashitaka wa
takukuru Bw.Kelvin Marusuri ameieleza mahakama kuwa mnamo june 7/ 2009 na September 21/2009 wakiwa ofisi za halmashauri ya wilaya walitumia
nyaraka kumdanganya mwajiri na kumsababishia hasara.
Watuhumiwa waliandaa nyaraka yenye
maelezo ya uongo kuwa kazi imefanyika kwa kuzingatia makubaliano na hivyo
mkandarasi anastahili kulipwa pesa zote
za mkataba licha ya kutambua kuwa kuna baadhi ya kazi za thamani ya tsh
10,326,200(milioni kumi laki tatu ishirini na sita elfu mia mbili)
hazikufanyika kulingana na mkataba.
Walihofikishwa mahakamani ni mhandisi,Mathias
Shoto akituhumiwa kwa kosa la kumdanganya mwajiri kinyume na kifungu cha 22 cha
sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007 na kumsababishia
mwajili hasara kinyume na kifungu cha 284a(1)cha kanuni ya adhabu sura 16
marejeo ya mwaka 2002.
Wengine ni Hamisi Allani Chande na
mkandarasi ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya Kidagaa,Bw.Peter Alexander.
Aidha mwandisi Mathias Shoto ameachiwahuru
kwa dhamana hadi kesi hiyo itakapotajwa
tena ifikapo march 10/2016 huku watuhumiwa Hamis Chande na Peter Alexanda
wakishindwa kukamilisha masharti ya dhamana na kwamba imeamuru warudishwe
mahabusu.
No comments:
Post a Comment