Halmashauri ya CCM Mkoa wa Geita imemvua ujumbe wa Mkutano Mkuu,
Peter Mwininga baada ya kudaiwa kukiuka maadili ya Umoja wa Vijana (UVCCM).
Licha ya kukiuka maadili ya umoja huo, Mwininga anadaiwa
kukisaliti chama hicho wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita kwa
kuwatukana viongozi wa ngazi za juu kwa njia ya mtandao.
Akizungumza baada ya kikao hicho juzi, Katibu wa Siasa na Uenezi
CCM mkoani hapa, Said Kalidushi alisema baada ya wajumbe wa halmashauri kuu
kupokea malalamiko na mapendekezo kutoka UVCCM, waliamua kumvua nafasi ya
ujumbe huo kutokana na kupungukiwa na sifa.
Kalidushi alisema wakati wa kampeni Mwininga alikihujumu chama
chao na kumfanyia kampeni mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa, huku akijua
wazi kuwa ni kosa.
Katibu wa UVCCM mkoani hapa, Mashaka Mshola alisema kitendo cha
Mwininga kuvuliwa nafasi aliyokuwa nayo kinatokana na usaliti na huo ni mwanzo
wa chama hicho kuwafukuza wasaliti
No comments:
Post a Comment