Friday 26 February 2016

SHIRIKISHO LA SOKA DUNIANI (FIFA) KUTANGAZA KIONGOZI MPYA LEO ATAEKUWA MRITHI WA SEPP BLATTER.


Blatter, 79, aliongoza shirikisho hilo tangu 1998. Aling’atuka mwaka jana kutokana na tuhuma za ufisadi zilizogubika shirikisho hilo. Kuna wagombea watano wanaotaka kumrithi.
Ambao  ni Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa, Gianni Infantino, Mwana mfalme Ali bin al-Hussein, Tokyo Sexwale na Jerome Champagne. Sheikh Salman na Gianni Infantino ndio wanaopigiwa upatu kushinda.
Upigaji kura utaanza saa 12:00 GMT (saa tisa alasiri saa za Afrika Mashariki) na Kabla ya kura kupigwa, kila mgombea atakuwa na dakika 15 za kuhutubia wajumbe,pia  kuna mataifa 209 wanachama wa FIFA lakini Kuwait na Indonesia kwa sasa hawashirikishwi, hivyo wajumbe watakaopiga kura ni 207.
Ili kutangazwa mshindi duru ya kwanza, mgombea anahitaji kupata theluthi mbili ya kura zilizopigwa. Hili lisipofanyika, wagombea wote wanapigiwa kura tena duru ya pili na atayepata kura nyingi kutangazwa mshindi.

Mshindi akikosekana duru ya pili, basi duru ya tatu hufanyika bila mgombea mwenye kura chache zaidi raundi ya pili, Fifa imesema lazima mshindi ajulikane leo Ijumaa.

No comments:

Post a Comment