Wasira Akimfuata mpiga picha kwa lengo la kufuta picha alizopigwa.
Mwanasiasa mkongwe nchini, Steven Wasira jana alimvamia mpiga picha
aliyekuwa akichukua picha zake wakati akitoka mahakamani, lakini akashindwa
kutimiza azima yake ya kufuta picha.
Wasiran ambaye ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika wa
Serikali ya Awamu ya Nne alifanya kitendo hicho akitoka kwenye jengo la
Mahakama ya Biashara ambako maombi yake ya kukata rufaa ya kupinga matokeo ya
uchaguzi wa ubunge, jimbo la Bunda yalitupiliwa mbali na Mahakama Kuu.
Katika kinyang’anyiro hicho cha ubunge, Wasira ambaye amekuwa mbunge wa Mwibara tangu mwaka
1970 na baadaye mbunge wa Bunda hadi mwaka 2015, aliangushwa na Ester Bulaya wa
Chadema katika uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana. Waandishi kutoka vyombo
mbalimbali vya habari akiwamo walishuhudia tukio hilo.
“Baadaye alitaka kumgonga kwa gari lake wakati akiondoka lakini ikashindikana.”
Akisimulia tukio hilo, Jamson alisema Wasira, ambaye amefanya
kazi na serikali za awamu zote tangu katikati ya miaka ya 70, alichukizwa na
kitendo chake cha kumpiga picha.
“Njoo, njoo hapa wewe
kijana. Nakuambia futa hizo picha kwa usalama wako.Hivi mnatafuta nini maana
mnanifuatilia tangu nikiwa kule Mahakama Kuu hadi huku Mahakama ya biashara,” alisema Wasira
Jitihada za Wasira kumnasa Jamson ziliendelea hadi nje ya eneo
la mahakama ambako alimfuata kwa kutumia gari aina ya Toyota Land Cruiser
(namba tunazihifadhi).
Katika kumfuatilia, gari la Wasira nusura limgonge mpigapicha
huyo, lakini waandishi wenzake walimnusuru kwa kumsukumia pembezoni mwa
barabara.
Juhudi za kumpata Wasira kuzungumzia sababu za kutaka
kumshambulia mpiga picha huyo kwa kuchukua picha za tukio hilo, hazikuzaa
matunda.
No comments:
Post a Comment