Wakizindua Kituo hicho.
Wakizindua huduma hiyo
na majengo ya kisasa waziri wa Tanzania anayeshughulikia Nchi za nje,
ushirikiano wa Afrika Mashariki kikanda na ushirikiano wa kimataifa Balozi
Agustin Mahiga na Phyillis Kandie ambaye ni Waziri wa Kazi na Afrika Mashariki
upande wa Kenya wamesema huduma hii iliyozinduliwa ni msingi muhimu katika
kuelekea kwenye Ushirikiano imara wa Afrika Mashariki.
Waziri Kandie amesema
kuweka huduma za Mpaka wa Nchi yani (one border post) katika mpaka wa Holili(Tanzania) na Taveta(Kenya) katika eneo moja kutakuza uchumi wa nchi
zote mbili kwa haraka.
Balozi Mahiga wa
Tanzania amesema hii ni moja ya hatua mojawapo za kuelekea katika matumizi ya
sarafu moja.
Mfano wa faida za
mradi kama huu ni unaona itapunguza takribani 400 (barabara ikikamilika kutoka
Mombasa kwenda Burundi) japo Gharama ni kufikia milioni 12 dola za kimarekani
lakini Afrika Mashariki tutafaidika" Ameongeza Katibu Mkuu wa Mtangamano
wa Afrika Mashariki Richard Sezibera aliyekuwepo kushuhudia ufunguzi huu.
Mradi huu ambao
umechangiwa na Nchi wahisani pamoja na Kenya na Tanzania umesimamiwa na Trade
Mark East Africa.
No comments:
Post a Comment