Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. john pombe magufuli amefanya uteuzi wa
mabalozi 3 katika wizara ya mambo ya nje, ushirikiano wa afrika mashariki,
kikanda na kimataifa. Magufuli pia amefanya uteuzi wa makamishna 4 wa jeshi la
polisi na kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA).
Taarifa
ya katibu mkuu kiongozi balozi Ombeni Sefue, imewataja mabalozi walioteuliwa
kuwa ni Dkt. Asha-rose Mtengeti Migiro, Mh Mathias Meinrad Chikawe na Dkt.
Ramadhan Dau.
Vituo
vya uwakilishi kwa mabalozi hawa vitajulikana baada ya taratibu husika za
kidiplomasia kukamilika.
Kwa
upande wa makamishna wa polisi, balozi Sefue amewataja walioteuliwa kuwa ni:
naibu
kamishna wa polisi Simon Nyakoro Sirro ambaye amepandishwa cheo kuwa kamishna
wa polisi, na ameteuliwa kuwa kamanda wa polisi kanda maalum ya dar es salaam.
kamishna Sirro anajaza nafasi iliyoachwa wazi na kamishna mstaafu Suleiman Kova.
Naibu
kamishna wa polisi Albert Nyamuhanga ambaye amepandishwa cheo kuwa kamishna wa
polisi na ameteuliwa kuongoza idara ya fedha, utawala na lojistiki.
Kamishna nyamuhanga anajaza nafasi iliyoachwa
wazi na kamishna wa polisi Clodwing Mathew Mtweve aliyeteuliwa kuwa katibu
tawala wa mkoa wa mwanza.
Naibu
kamishna wa polisi Robert Boaz Mikomangwa ambaye amepandishwa cheo kuwa
kamishna wa polisi na ameteuliwa kuongoza idara ya intelijensia.
Kamishna
Mikomangwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na kamishna Valentino Mlowola aliyeteuliwa
kuwa kaimu mkurugenzi mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (takukuru).
Kamishna
msaidizi mwandamizi wa polisi Nsato Marijani Mssanzya ambaye amepandishwa cheo
kuwa kamishna wa polisi na ameteuliwa kuongoza idara ya mafunzo na
operesheni.
Kamishna
msanzya anajaza nafasi iliyoachwa wazi na kamishna wa polisi Paul moses Chagonja
aliyeteuliwa kuwa katibu tawala wa mkoa wa katavi.
aidha,
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Modestus
Francis Kipilimba kuwa kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya vitambulisho vya
taifa (NIDA).
kabla
ya uteuzi huu Dkt. Kipilimba alikuwa mkurugenzi wa menejimenti ya udhibiti
(director of risk management) katika benki kuu ya Tanzania na hivyo Dkt.
kipilimba anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Dikson Maimu ambaye uteuzi wake
ulitenguliwa.
teuzi
zote zimeanzia jana tarehe 15 februari, 2016
No comments:
Post a Comment