Naibu waziri wa madini Staslaus
Nyongo Akizungumza na mmoja wa wamiliki wa mgodi huo Bw ,Alex Kindersley.
Naibu Waziri wa madini Stanslaus Nyongo
amewataka wamiliki wa mgodi wa Nyarugusu Mine Company kuwalipa fidia haraka iwezekanavyo wananchi 133 ambao wapo
kwenye kijiji cha Ziwani kata ya Nyarugusu Wilayani Geita kutokana na kuharibiwa
mazao yao na sumu ambayo ilitoka kwenye Bwawa la maji yenye sumu.
Agizo hilo ambalo amelitoa Naibu waziri
wa madini Nyongo limetokana na Wananchi hao ambao wanadai kulipwa fidia ya
kiasi cha sh,milioni 202 kufunga barabara ya mgodi huo tangu Februari 18,mwaka
huu kufuatia Mgodi huo kutoa majibu yenye utata.
Bi, Pili Ramadhani alisema walipatwa na
majanga hayo novemba 30 mwaka jana baada ya mazao yao kuharibiwa,na
kwamba wamekuwa wanakabiliwa na njaa,hali ambayo imesababisha kuhamua
kuandamana huku wakikaa takribani wiki nzima kwenye maeneo ya nje ya mgodi huo
wakiitaji walipwe madai yao.
Mzee Slvanus Matanywa (88) mkazi
wa kijiji cha ziwani amejikuta akiangua kilio mbele ya Naibu Waziri wa Madini
Stanslaus Nyongo akililia fidia yake kutokana na kukabiliwa na njaa kwa kukosa
chakula baada ya mazao yake kuharibiwa na sumu hiyo.
“Nalia kwasababu wajukuu wangu awasomi kutokana na kulala na njaa
kwanini imekuwa namna hiyo sasa sijui nifanyeje sina chochote cha
kunisaidia watoto wakianza kulia nashindwa nifanye nini wewe ndiyo Baba maana
tumeambiwa tuheshimu mamlaka iliyo juu” Alisema Mzee Matanywa.
Nae Mwenyekiti Wa Kijiji hicho
Athuman Seleman alisema ni kweli wananchi wake tangu November mwaka
jana mashamba yao yaliingiliwa na matope yenye sumu na serikali imeendelea
na jitihada za awali za kufanya mazungumzo na mgodi ili
walipe fidia shida ilikuja baada ya wamiliki wa mgodi kuleta barua
ya kusema hawawezi kutoa fidia kwa sasa mpaka wajiridhishe kutokana na
vipengele fulani hapo ndio lililipokuja tatizo.
“Shida iliyokuja
ni kutokana na mgodi kugoma kutoa fidia kwa madai wanataka baadhi ya vipengere
wajiridhishe suala hili limewakwanza wananchi na kweli kabisa mheshimiwa watu
awa wanashida sanaa na maisha yao yote walikuwa wanategemea mazao ambayo yanapatikana
kwenye mashamba yao na maamuzi ya kufunga mgodi yamekuja ni baada ya
kukasirishwa na majibu ya mgodi” Alisema Mwenyekliti.
Kufuatia malalamiko hayo waziri wa
Madini Mh.Stanslaus Nyongo ameunga mkono hatua iliyochukuliwa na wananchi wa
Kijiji hicho kwa kufunga barabara inayoingia kwenye Mgodi kutokana
na kuwepo kwa majibu ambayo yamekuwa yakitolewa ya kukatisha tamaa.
‘’
Naomba istafsiliwe mlichokifanya ni makosa kufunga au kuzuia njia hii ya
kuingia mgodini mmefanya sawa sawa kwa sababu mnadai haki yenu, nilikuwa
namtafuta uyu mzungu toka jana lakini ninataarifa polisi wamemkamata tayari’’
Alisema Nyongo.
Akizungumza na mmoja wa wamiliki wa
mgodi Bw ,Alex Kindersley Naibu waziri Nyongo amewataka kwa
kushilikiana na mkuu wa wilaya ya Geita kumaliza tatizo hilo ndani ya
wiki moja kulipa madai ya wananchi hao tofauti na hivyo kama wizara
watachukua hatua za kinidhamu dhidi ya mgodi .
|
No comments:
Post a Comment