Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Geita,Khadja Said akiwakilisha Bajeti ya mwaka 2018/19. |
Katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita kikao cha baraza la
madiwani kiliongozwa na Mheshimiwa Hadija Said Makamu
mwenyekiti wa Baraza hilo na kuhudhuriwa na Mbunge wa jimbo la Busanda
Mheshimiwa Lolensia Bukwimba, Waheshimiwa Madiwani, Wataalam wa Halmashauri,
Viongozi wa vyama vya siasa na wadau wengine wa maendeleo kutoka wilayani hapa.
Katika bajeti hiyo shilingi bilioni 18,040,010,550/= ambazo
ni fedha za ruzuku zitatumika kutekeleza miradi ya maendeleo, Shilingi
bilioni 2,440,501,771/= ni fedha za ruzuku zitakazotumika kwa matumizi ya
kawaida (OC),Shilingi bilioni 53,607,008,000/= zitatumika kulipa
mishahara, shilingi bilioni 3,585,714,500/= ni makusanyo
ya ndani, shilingi bilioni 1,297,941,800/= ni matumizi ya kawaida ya
mapato ya ndani (OS) na Shilingi bilioni 2,084,412,700/= zitatumika
kutekeleza miradi ya maendeleo, shilingi milioni 203,360,000/= ni
matumizi ya mapato mengine ambayo ni (CHF,NHIF/User fee) na shilingi
bilioni 1.5 zitakuwa ni nguvu za wananchi kuchangia miradi ya maendeleo.
Sambamba na hilo Halmashauri imeainisha chanzo kipya cha mapato
ambacho ni kituo cha redio cha rubondo kinachotarajiwa kuanza kazi hivi
karibuni kukasimiwa katika bajeti na kukadiriwa kuingiza kiasi cha shilingi milioni
250.
Bajeti hii ina matarajio makubwa ya kuboresha huduma za jamii
kupitia sekta za Elimu, Afya, Maji,Ardhi na Mifugo, Pia Kuboresha miundombinu
ya ufundishaji na kufundishia mashuleni kwa kujenga shule za elimu ya
juu(A’Level), Hosteli za wasichana, Vyumba vya madarasa,Nyumba za walimu,
Maabara na kutoa Motisha kwa walimu kwa lengo la kuongeza ufanisi.
No comments:
Post a Comment