Naibu Waziri wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kushoto) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde (Kulia) wakifatilia taarifa ya Mkoa wa Shinyanga mara baada ya kuwasili Mkoani humo kwa ziara ya kikazi, Leo 27 Februari 2018.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Bi Haula Kachwamba akizungumza jambo mara baada ya Naibu Waziri wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kulia) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde (Kushoto) kuzuru katika ofisi za chama wakiwa katika ziara ya kikazi, Leo 27 Februari 2018.
Naibu Waziri wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo mara baada ya kuwasili Mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi akiwa sambamba na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde, Leo 27 Februari 2018.
Naibu Waziri wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko na Naibu Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde leo 27
Februari 2018 wametinga Mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi ya siku moja
ambapo pamoja na mambo mengine watatembelea mgodi wa EL-Hillal Minerals Ltd.
Mhe Biteko ametinga Mkoani Shinyanga akitokea ziarani Mkoani Tabora huku
Mhe Mavunde akiwa ametokea Mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa
maelekezo ya ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi mwaka 2015-2020.
Wakati Mhe Mavunde akiwa kwenye ziara ya kukagua Viwango vya Kazi na
Usajili wa waajiri kwa mfuko wa fidia wa wafanyakazi (WCF) ni sehemu ya kukagua
Viwango vya Kazi na kufuatilia utekelezaji wa agizo la Mhe Jennister
Mhagama ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na
Ajira ambaye aliwataka waajiri wote nchini wawe wamejisajili kwenye mfuko
wa Fidia wa Wafanyakazi kabla au ifikapo tarehe 30 Septemba 2017.
Amesisitiza waajiri kujisajili na mfuko wa fidia kwa wafanyakazi kwani
kutofanya hivyo Kwa mujibu wa Kifungu cha 71(4) atashitakiwa Mahakamani na
akikutwa na hatia adhabu yake ni faini isiyozidi TSh 50,000,000 au kifungo cha
miaka mitano au vyote kwa pamoja.
Wakati huo huo Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amesisitiza
umuhimu wa wachimbaji wadogo nchini kulipa kodi huku akieleza kuwa wachimbaji
wanapaswa kujiunga kwenye vikundi kwani serikali imetenga maeneo mengine ambayo
itatoa wataalamu kuyafanyia Utafiti ili kuimarisha uchimbaji nchini kwa
wachimbaji wadogo kuwa wenye tija na hatimaye kuwafanya kutoka katika uchimbaji
mdogo kufikia wa kati na hatimaye kuwa wachimbaji wakubwa.
Pia ameendelea kusisitiza juu ya Wamilili wa Leseni za Madini kote
nchini, kutunza takwimu za gharama za uendeshaji wa shughuli zao za uchimbaji
na kila Mwezi ziwasilishwe kwa Afisa Madini kwani kutokufanya hivyo wataingia
katika mikono ya sheria kwa kulipa faini ya shilingi milioni 50 mpaka milioni
150 au kifungo cha mwaka mmoja jela.
Pia, Mhe Biteko ameeleza dhamira ya ziara yake kuwa anapokuwa katika
maeneo mbalimbali anawakumbusha wachimbaji nchini kufuata sheria na taratibu za
nchi.
No comments:
Post a Comment