Na,Joel Maduka ,Chato
Waziri wa Nishati,Dkt Medard Kalemani
amemwagiza mkandarasi shirika la White City Internationala mbaye
anasambaza umeme wa rea awamu ya tatu kwenye Vijini na kata za Iparamasa na
Kalembela kuhakikisha anafanya kazi hiyo kwa haraka zaidi ili kuwasaidia
wananchi ambao wamekuwa na kilio cha muda mrefu cha uhitaji wa nishati ya umeme.
Hayo aliyasema wakati alipokuwa kwenye
ziara ya Kukagua na kuangalia utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme
vijijini Wilayani Chato.
Ambapo Diwani wa kata ya Iparamasa
Amos Jiji ,amemweleza Waziri wa nishati ambaye pia ni mbunge wa Jimbo hilo matatizo
ambayo yameendelea kujitokeza kutokana na kukosekana kwa umeme
kwenye kata yake na kwamba kwa sasa kuna nguzo ambazo zimekaa kwa
muda wa miezi mitatu bila ya kusambazwa kwa wananchi ambao wanashida na huduma
hiyo.
Mmoja kati ya wananchi wa kata
hiyo ,Bw Peter Mabula ameelezea kukosekana kwa umeme ni chanzo kikubwa ambacho
kinakwamisha utendaji kazi hususani kwa upande wa biashara kutokana na wengi
wao kutegemea nishati hiyo ili waweze kuendesha biashara zao.
Aidha kutokana na maombi hayo kutoka
kwa Diwani pamoja na wananchi Mbunge wa Jimbo la Chato na waziri wa nishati Dk
Kalemani alitoa maagizo kwa Mkandarasi kuhakikisha nguzo ambazo zimelala
ndani ya miezi mitatu zisimame na kufikia siku ya alhamisi vijiji hivyo na kata
hizo ziwe zimepata umeme.
“Nimesikia kuwa nguzo zimelala tu
chini ndani ya miezi mitatu na kwamba mkandarasi alivyosikia nakuja ndio
ameanza kazi sasa namwagiza kuwa ahakikishe alhamisi wiki ijayo awe amewasha
umeme kwenye kata ya iparamasa na vijiji vyote na mimi siondoki hapa
nitahakikisha namsimamia”Alisisitiza Kalemani.
Mradi wa usambazaji wa umeme
vijijini Mkoani Geita,unatekelezwa na mkandarasi wa Shirika la
White City International ambapo unatarajia kufanyika ndani ya miezi
16 kwenye jumla vijiji 220 vilivyopo mkoani humo na jumla ya
fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza mradi huo ni Sh Bilioni
78.56.
No comments:
Post a Comment