Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akibadilishana
mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shighella mara baada ya kumaliza
mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa kabla ya Naibu
Waziri huyo ajaanza kukagua miradi ya barabara katika Wilaya za Pangani na
Muheza jana Jumanne Februari 13, 2018.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiiaino, Elias Kwandikwa akizungumza na
Viongozi na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga
wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya barabara katika
Wilaya hiyo jana Jumanne Februari 13, 2018. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya
Pangani, Bi. Zainab Issa.
Meneja wa
TANROAD Mkoa wa Tanga, Mhandisi Alfred Ndumbaro akitoa maelezo ya
ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias
Kwandikwa (wa pili kulia)kuhusu ujenzi wa Daraja kubwa lenye urefu wa
kilometa 550 linalotarajia kujengwa na Serikali katika Mto Pangani wakati
wa ziara yake Wilayani humo jana Jumanne Februari 13 2018. Kulia ni Mkuu
wa Wilaya hiyo, Bi. Zainab Issa.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akipata maelezo
kuhusu ufafanisi wa utendaji kazi wa kivuko cha MV Tanga wakati wa ziara
yake ya kukagua miradi ya barabara na vivuko katika Wilaya ya Pangani na
Mkoa wa Tanga kwa ujumla katika ziara yake jana Jumanne Februari 13 2018.
Kulia ni Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme Serikalini (TEMESA), Mhandisi Magreth
Ginna.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akishuka katika
kivuko cha MV Tanga iliyopo Pangani wakati wa Ziara yake ya kukagua miradi
mbalimbali ya barabara na vivuko katika Wilaya za Mkoa wa Tanga jana
Jumanne Februari 13, 2018. Anaongoza nao Diwani wa Kata ya Pangani
Magharibi, John Semhande na Meneja wa TEMESA Mkoa wa Tanga, Mhandisi
Magreth Ginna na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Zainab Issa.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa amesema Serikali imekusudia kuimarisha sekta ya ujenzi na uchukuzi katika Mkoa wa Tanga ikiwemo Ujenzi wa Daraja kubwa lenye urefu wa Mita 550 katika Wilaya ya Pangani, hatua inayolenga kufungua fursa na kuinua pato la kiuchumi kwa wanachi wa Mkoa huo.
Akizungumza katika mkutano wake na Mkuu wa
Mkoa huo, Martin Sheghela jana Jumanne Februari 12, 2018, Naibu Waziri
Kwandikwa aliyopo katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya barabara Mkoani
humo, alisema lengo la Serikali ni kuimarisha miundombinu ya barabara, bandari
na uwanja wa ndege katika Mkoa wa Tanga.
Kwandikwa alisema katika bajeti ya mwaka
2017/18 Serikali imekusudia kuanza ujenzi wa barabara ya
Tanga-Pangani-Saadani-Bagamoyo yenye urefu urefu wa kilometa 242, ambapo tayari
kazi ya usanifu wa barabara hiyo tayari umeaanza, ambapo wakati wowote kutoka
sasa Serikali inatarajia kutangaza zabuni ya ujenzi wa barabara hiyo.
“Kwa kipande cha barabara ya Tanga-Pangani
ambayo imekuwa kilio cha wananchi wa Pangani kwa kipindi kirefu, tayari
tumeanza hatua ya usanifu wa barabara hiyo, ambapo Serikali imetenga kiasi cha
Tsh. Bilioni 4.3 kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo” alisema Kwandikwa.
Aliongeza kuwa Serikali pia
imepanga kuharakikisha ujenzi wa Barabara ya Handeni-Kilindi-Nchemba-Mkoro
yenye urefu wa kilometa 461 ambayo inatarajia kuunganisha Wilaya ya Kondoa na
Mkoa wa Singida, hatua inayolenga kuongeza fursa ya shughuli za uzalishaji mali
kwa kuzingatia fursa ya ujenzi wa bomba la mafuta linloatarajiwa kuanza ujenzi
wake mwaka huu.
Kuhusu ujenzi wa uwanja wa ndege na
uimarishaji wa bandari ya Mkoa wa Tanga, Naibu Waziri Kwandikwa
alisema uwezeshaji na utekelezaji wa ujenzi na ukarabati
wake upo katika miradi ya Afrika Mashariki, ambapo kukamilika kwake
kutasaidia kuzalisha ajira na kuongeza mvuto wa Mkoa wa Tanga kwa wawekezaji
mbalimbali.
Kwa mujibu wa Kwandikwa alisema mbali na Mkoa
wa Tanga, Serikali imekusudia kutekeleza miradi mbalimbali ya barabara nchini
kwa wakati hatua inayolenga kuwapunguzia gharama wananchi na kuokoa muda wa
kusafirisha bidhaa na malighafi.
“Ujenzi wa Barabara ya
Handeni-Kilindi-Nchemba-Mkoro ukikamilika unatarajia kuokoa zaidi ya kilometa
150 kwa abiria wanaosafiri kutoka Dar Es Salaam hadi Singida, huu ni mradi
muhimu na hivyo tutaupa kipaumbele cha pekee” alisema Kwandikwa.
Kwa upande wake Mkuu wa MKoa wa Tanga, Martin
Sheghella alisema ujenzi wa miundombinu ya uhakika ikiwemo uimarishaji wa
bandari ya Tanga katika Mkoa huo utasaidia kuongeza pato la wananchi na
mapato ya Serikali kwa kujenga ushawisihi wa Nchi jirani ikiwemo Burundi,
Rwanda, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutumia Bandari hiyo.
“Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya Shehena za
mizogo Milioni 28 zinasafirishwa katika nchi jirani za Burundi, Rwanda, Uganda
na DRC lakini iwapo tutaimarisha bandari ya Tanga tutaweza kukifanya nchi hizi
zikatumia bandari yetu” alisema Sheghella.
No comments:
Post a Comment