Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan akiongea na wadau wa Elimu Mkoani Simiyu, leo wakati wa Kongamano
kubwa la Elimu ya Juu lililoandaliwa na Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa
kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka
akimuelezea Makamu wa Rais (hayupo pichani) namna utekelezaji wa mpango wa EQUIP-Tanzania unavyofanyika
mkoani humo katika kongamano la Elimu ya Juu lililofanyika leo, mkoani humo.
Mkuu wa DFID-Tanzania Bibi Elizabeth Arthy
akizungumza mbele ya Makamu wa Rais juu ya mchango wa Serikali ya Uingereza
katika kuboresha elimu nchini Tanzania katika kongamano la Elimu ya Juu
lililofanyika leo, mkoani Simiyu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaagiza watalaamu wa elimu na viongozi wa
Mkoa wa Simiyu kuhakikisha wanaendeleza Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu
Tanzania (EQUIP-Tanzania) unaotekelezwa na Serikali kwa ushirikiano na Shirika
la Maendeleo la nchini Uingereza (DFID).
Makamu wa Rais
ametoa agizo hilo leo Mkoani Simiyu alipokuwa akiongea na viongozi na watumishi
wa Serikali wa Mkoa huo katika kikao cha
majumuisho ya ziara yake ya siku tano mkoani humo.
"Mpango huu umekuwa na mafanikio makubwa kwa Mkoa
wa Simiyu, kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu wa wanafunzi katika mitihani
ya kitaifa ya darasa la Saba ambapo Mkoa umetoka kushika nafasi za mwisho Kitaifa
hadi kufikia nafasi ya 11 mwaka 2017.
Amesema mafanikio ya mpango huo yamekuwa makubwa, huku akishukuru shirika la DFID kwa mchango wao mkubwa ikiwa ni pamoja na kutoa kiasi cha fedha shilingi Bilioni 1.3 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule.
Aidha, Mhe. Samia ameutaka uongozi wa mkoa huo kuhakikisha Mpango huo unaendelezwa hata baada ya wafadhili hao kumaliza muda wao ili kuhakikisha kiwango cha elimu kinaendelea kuboreka kila mwaka.
Amesema mafanikio ya mpango huo yamekuwa makubwa, huku akishukuru shirika la DFID kwa mchango wao mkubwa ikiwa ni pamoja na kutoa kiasi cha fedha shilingi Bilioni 1.3 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule.
Aidha, Mhe. Samia ameutaka uongozi wa mkoa huo kuhakikisha Mpango huo unaendelezwa hata baada ya wafadhili hao kumaliza muda wao ili kuhakikisha kiwango cha elimu kinaendelea kuboreka kila mwaka.
Mhe. Samia amemuhakikishia Kiongozi Mkuu
DFID-Tanzania Bibi Elizabert Arthy kuwa nchi ya Uingereza itaendelea kufanya
kazi na Serikali katika kuboresha elimu nchini.
Kwa upande wake, Elizabeth Arthy amesema katika kuhakikisha wanapambana na hali ya kuboresha elimu nchini tayari Mkoa wa Simiyu umepewa fedha kutoka DFID kiasi cha shilingi Bilioni 1.3 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka ameishukuru
DFID kwa ufadhili wake kupitia EQUIP-Tanzania ambapo ufaulu wa wanafunzi umeongezeka
mkoani humo kutoka asilimia 36 mwaka
2013 mpaka 68 mwaka 2017.
Katika kipindi cha miaka Minne DFID imewekeza katika
mpango wa kuinua ubora wa elimu mkoani Simiyu kwa kutoa kiasi cha Shilingi Bilioni
9.
No comments:
Post a Comment