Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,Mponjoli Mwabulambo akizungumza na waandishi wa habari juu ya tukio la kufariki kwa mtoto wakati alipokuwa akiombewa.
Mtoto wa miaka sita (6) ambaye anajulikana kwa jina la Frank Bariki
amefariki wakati alipokuwa akiombewa mlimani alikopelekwa kwaajili ya kutolewa
mapepo kwa madai alikuwa na taswira ya Bibi yake,huku mama mzazi
akishikiliwa na jeshi la polisi kwaajili ya upelelezi.
Kamanda wa Polisi mkoani Geita,Mponjoli Mwabulambo alisema Tukio hilo
lilitokea february 18,2018 majira ya saa tano asubuhi katika mlima wa
Gambiwe kwenye kijiji cha Bukuru Wilaya ya Nyang’hwale.
Aidha amewataja wanawake hao kuwa Bi,Neema Petro(25) ambaye
ni mama wa mtoto huyo na mke mwenzake Raheli Mussa (25) ambao
wameolewa na Bw,Bariki Lunyaru walikuwa kwenye kipindi cha mfungo wakiwa kwenye
maombi yao wakati wakimuombea kwaajili ya kumtoa mapepo ndipo walianza kumkamia
mtoto huyo wakimshika na kumkaba kwenye mbavu na kwenye shingo hali ambayo
ilipelekea mtoto huyo kupoteza maisha.
Kamanda Mponjoli ameendelea kusema wamechunguza mwili wa mtoto
wamebaini kulikuwa na alama za mikwaruzo kwenye maeneo ya shingoni
na kwenye mashavu .
Ameendelea kufafanua kuwa hadi sasa bado hawajajua
kiini cha tukio hilo ambalo limesababisha mtoto huyo kupoteza uhai
wakati alipokuwa akifanyiwa maombi ingawa hadi sasa jambo ambalo wamebaini
kuna viashiria vya vitendo vya ushirikina ndani ya familia kutokana na
madai ya taswira ya bibi yake .
Kamanda Mponjoli alisema hadi sasa wanawashikilia wanawake hao
ambao ni wakazi wa kijiji cha Bukulu wilayani Nyang’hwale kutokana na kifo cha
mtoto huyo.
|
No comments:
Post a Comment