Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili Jijini
Mwanza jana jioni na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka.
Makamu wa Rais anategemewa kuanza ziara ya kuhamasisha
shughuli za kimaendeleo kesho mkoani Simiyu.
Pia Makamu wa Rais ataweka jiwe la msingi kwa
ajili ya ujenzi wa nyumba za viongozi wa mkoa katika eneo la Nyaumata.
Miradi mingine ambayo Makamu wa Rais
ataitembelea ni Kukagua Ujenzi wa Barabara za Lami Bariadi mjini chini ya
Programu ya uimarishaji wa Serikali za Mitaa za Mjini.
Makamu wa Rais atakagua maendeleo ya ujenzi wa
bwawa la Mwanjoro na kusalimia wananchi siku ya tarehe 20, pia atasalimia
wananchi wa Mwanhuzi Mjini, Mwandoya (Meatu).
Tarehe 21, Makamu wa Rais atafungua Kongamano
la Elimu ya Juu na Uchumi wa Viwanda Tanzania kasha atafungua jengo la Utawala
la halmashauri ya Itilima na kusalimia wananchi, kufungua jingo la upasuaji la
Samia Suluhu Hassan katika Hospitali ya Wilaya ya Maswa na kuzungumza na
wananchi katika viwanja vya nguzo nane.
Siku ya tarehe 22, Makamu wa Rais ataongoza
Mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu Huria.
No comments:
Post a Comment