Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipakwa majivu wakati wa ibada ya
Jumatano ya Majivu katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam
asubuhi ya leo.
RAIS wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameungana na waumini wa Kanisa
Katoliki na wakristo wengine katika ibada ya Jumatano ya majivu inaoashiria
kuanza kwa mfungo mtukufu wa kwaresma.
Magufuli akiwa na
mkewe, Mama Janeth Magufuli wameungana na waumini hao katika ibada iliyoongozwa
na Muadhama Askofu Mkuu, Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam
katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Dar, leo Februari 14, 2018.
Rais John Magufuli
akisalimiana na Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la
Dar es Salaam baada ya kujiunga na waumini wengine katika ibada ya Jumatano ya
Majivu katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam asubuhi ya leo
Feb 14.
Mama Janeth Magufuli
akisalimiana na Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la
Dar es Salaam baada ya kujiunga na waumini wengine katika ibada ya Jumatano ya
Majivu katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam asubuhi ya leo Feb
14.
No comments:
Post a Comment